Asha Kigundula
Ofisi za TFF |
Tukio hilo lilitokea jana saa
8, mchana baada ya maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Ilala na
kampuni ya udalali ya Yono, kufika katika ofisi hizo na kuamuru wafanyakazi
watoke na wao kuamua kufunga ofisi hizo.
Ofisa mmoja wa TFF ambaye
hakutaka jina lake litajwe, jana aliliambia Jambo Leo maofisa hao walipofika
katika ofisi hizo waliwaambia watoke, nao wakatii kabla ya kufunga.
Alisema hatua hiyo imechukuliwa
wakati Jumatatu wiki hii viongozi wa juu walipunguza deni kwa kulipa sh.milioni
250, kisha sh. milioni 40 siku iliyofuata.
TRA awali Machi 31 mwaka jana
ilikamata magari matano ya TFF pamoja na kufungia akaunti za TFF ambazo
zilikuwa na fedha zaidi ya sh. milioni 400 ambazo zilichukuliwa kwa ajili ya
kufidia deni hilo.
Deni hilo la sh. milioni 1.6
lilitokana na kodi ya mechi kati ya Tanzania na Brazil iliyoandaliwa na
serikali, ikiwa ni pamoja na kodi za mishahara ya makocha wakigeni ambao
waliwahi kufundisha timu za Taifa, Taifa Stars.
Mwaka jana zilipofungwa akaunti
hizo, kikosi cha timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17 (Serengeti Boys)
kilichokuwa katika safari yake kwa ajili ya michezo ya kirafiki katika nchi za
Burundi na Rwanda kiliahirisha kutokana na kukosa posho za wachezaji na
gharama za kambi.
Kwa sasa Serengeti Boys iko
kambini kujiandaa kushiriki mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon)
yatakayofanyika Gambia Mei mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment