Dotto Mwaibale
Soko la Feri |
ENEO la Lebanon katika soko la kimataifa
la samaki la Feri, Dar es Salaam, limeelezwa kuongoza kwa vitendo vya ukatili wa
kijinsia hasa dhidi ya watoto.
Hayo yalielezwa na Mwenyekiti wa Soko
hilo, Ali Bunda alipozungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana wakati
akitoa taarifa ya kupungua kwa ukatili wa kijinsia katika soko hilo baada ya
kupata mafunzo kutoka Shirika la Equality for Growth (EfG).
"Vitendo vya ukatili wa kijinsia
vimepungua kwa kiasi kikubwa katika maeneo mengine ya soko letu, lakini
changamoto kubwa ipo Lebanon, huko ukipita usiku unaweza kulia kutokana na
vitendo vinavyofanyika," alisema Bunda.
Alisema katika eneo hilo kila vitendo
vichafu vimekuwa vikifanyika kwani hivi karibuni kuna mwanamume alikamatwa akimlawiti
mtoto wa kiume na alipofikishwa kituo cha Polisi mtoto huyo aliomba mwanamume
huyo asipelekwe mahakamani, kwani ni msaada mkubwa kwake kwa kuwa amekuwa
akimpa fedha za chakula na mahitaji mengine.
"Kauli ya mtoto huyo ilimshitua
kila mtu aliyekuwa kituoni hapo lakini pamoja na maombi hayo, polisi
waliendelea kumshikilia ili sheria ichukue mkondo wake," alisema Bunda.
0 comments:
Post a Comment