Ibrahim Yassin, Mbozi
Chiku Galawa |
Serikali Kuu
ilitoa fedha za ruzuku kwa ajili ya shughuli za maendeleo wilayani humo mwaka
2011/12 ambazo zinadaiwa kutofanya shughuli kusudiwa na kuingizwa kwenye
akaunti isiyo ya Halmashauri na kutumika vibaya.
Wakati fedha
hizo zikiingia, Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo wakati huo alikuwa Levson
Chilewa na Mwenyekiti wa Halmashauri Erick Ambakisye ambaye hadi sasa
anaendelea na wadhifa huo.
Fedha hizo
zilizua utata mkubwa huku madiwani wakihoji matumizi yake ambapo Mkaguzi na
Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), alibaini kuwapo ubadhirifu huo.
Mwaka jana, Galawa
aliunda tume kubaini utata huo baada ya malalamiko ya madiwani ikabaini
ubadhirifu na kuamuru wahusika hata kama walistaafu waitwe kuhojiwa, kisha
kuchukuliwa hatua za kisheria.
Akizungumzia
hali hiyo jana, Galawa alitaja wahusika wakuu kuwa ni Chilewa ambaye amestaafu,
Mganga Mkuu (DMO) Charles Mkombachepa, Ofisa Mipango, Christopher Nyalubamba,
Ofisa Elimu Sekondari, Isaack Mgaya na Mhazini Mkuu, Rashid Mbegumoja.
Galawa alisema
baada ya tume kukamilisha uchunguzi ilibainika fedha hizo kupelekwa kwa wakuu
wa idara na kuamua waitwe kuhojiwa kisha wachukuliwe hatua stahiki na mwajiri wao ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Edina Mwaigomole ambaye yuko likizo ya kustaafu
aliliambia gazeti hili kwa njia ya simu, kuwa alipelekwa kufanya kazi kwenye Halmashauri
hiyo mwaka 2014 ambako alikuta tuhuma hizo huku akiwa hana mawasiliano na
mtangulizi wake, Chilewa.
Wananchi
walisema Halmashauri hiyo imekuwa na kashfa nyingi za ubadhirifu wa fedha za
maendeleo, hali inayosababisha kupata hati chafu zenye shaka kwa zaidi ya miaka
minne mfululizo, wakihimiza hatua zichukuliwe haraka au Halmashauri hiyo ifutwe
kuliko kugeuzwa ‘shamba la bibi’.
0 comments:
Post a Comment