Emeresiana Athanas
Kamanda Sirro |
WAKAZI 15 wa Dar es Salaam, wanatarajiwa kufikishwa mahakamani
baada ya kukamatwa na Polisi, kwa tuhuma za kukiuka amri ya Mahakama ya kuhama
maeneo hatarishi ya mabondeni.
Mbali na hao, Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, pia
limemhoji Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Msongela Palale baada
ya kulalamikia uvamizi wa maeneo ya mabondeni.
Akizungumza jana, Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Simon Sirro,
alisema watu hao walikamatwa kwenye oparesheni Buguruni kata ya Vingunguti.
Kamanda Sirro alitaja baadhi yao kuwa ni Mohamed Hatibu, Mwanaidi
Mwinyimvua, Kurwa Anthony, Mwanahamisi Athuman na Saada Saidi.
“Katika mahojiano na watu hawa, walikiri kuendelea kuishi kwenye
maeneo hatarishi mabondeni na kwamba wanasubiri maelekezo kutoka serikalini na
upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani,” alisema.
Aidha, Jeshi hilo kupitia Kikosi cha Usalama Barabarani
limekusanya Sh milioni 319.35 kutokana na tozo za barabarani katika makosa 10,249
ya usalama barabarani.
Kamanda alisema fedha hizo zilipatikana kati ya Machi 14 na 16.
0 comments:
Post a Comment