Suleiman Msuya
Profesa Lipumba na Maalim Seif |
BARAZA Kuu la CUF limewasilisha majina
ya wajumbe wa Bodi yake mpya ya wadhamini kwa Wakala wa Usajili, Ufilisi na
Udhamini (Rita).
Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Uhusiano
wa Umma, Salim Biman alibainisha hayo jana katika taarifa iliyosambazwa kwa
vyombo vya habari.
Alisema mapendekezo ya uteuzi wa wajumbe
hao yalipokewa na Baraza Kuu la CUF kwenye kikao chake yakiwa ajenda namba 4(A)
ili kukidhi matakwa ya Katiba Mpya ya CUF toleo la mwaka 2014 Ibara ya 98(1),
(2), (3), (4), (5), na (6).
Diman alisema baada ya mjadala wa kina,
Baraza Kuu lilipitisha majina ya wajumbe tisa wa Bodi ambao ni Abdallah Khatau,
Ali Mbarak Suleiman, Mohamed Nassor Mohamed na Dk Juma Ameir Muchi.
Wengine ni Mwanawetu Said Zarafi, Blandina
Mwasabwite, Yohana Mbelwa, Mwana Masoud
na Zumba Kipanduka.
Mkurugenzi huyo alisema hatua hiyo ni
muhimu kwa chama iliyofanyika jana baada ya kukamilisha hatua zote za kikatiba za
CUF, sheria za nchi na mikakati ya kuimarisha chama ili kukabiliana na wenye
nia ovu dhidi ya CUF.
Alisema kikao hicho kilichofanyika Vuga,
Mjini Unguja, kilihudhuriwa na wajumbe
halali 43 kati ya halali 53 na wajumbe watano kati yao hawakuhudhuria kwa
udhuru kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo ya kuwa nje ya nchi.
“Uteuzi huu wa Bodi mpya haubatilishi uamuzi
wowote halali uliochukuliwa na Bodi ya awali na usajili huu umesimamiwa
kikamilifu na Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar,
Nassor Mazrui na Mkurugenzi wa Fedha na Uchumi ambaye pia ni Kaimu Naibu Katibu
Mkuu Bara, Joran Bashange,” alisema.
Usajili huo unakuja siku chache baada ya
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba kutangaza kuunda Bodi ya Wadhamini
mpya kwa madai iliyokuwapo muda wake umekwisha.
0 comments:
Post a Comment