Dalila Sharif
Felix Lyaniva |
MKUU wa
Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva, ametaka wananchi wa wilaya hiyo kuwa waangalifu
na wajiepushe na ulaji ovyo ili kuepuka magonjwa hatarishi kama kipindupindu.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi juzi Dar es Salaam, Lyavina alisema kutokana na ongezeko
la uuzaji na matumizi ya vyakula kwenye mazingira hatarishi, ni vema kila
mwananchi akazingatia usafi wa mazingira maeneo ya kazi hata katika uuzaji
bidhaa za vyakula wilayani humo.
Alisema
hali hiyo itasaidia kupunguza magonjwa hatarishi kikiwamo kipindupindu hivyo
kuokoa maisha ya watu.
“Kipindupindu
ni cha mlipuko, kinatokea wakati wowote kutokana na mazingira kuwa hatarishi hasa
katika kipindi hiki cha mvua,” alionya Lyaniva.
Alisema
uhifadhi na ununuaji wa vyakula salama utasaidia kupunguza magonjwa yanayoambukiza.
Lyaniva alitaka
wananchi wa wilaya hiyo kuwapa elimu watoto wao kununua vyakula vilivyo katika
hali ya usalama ili kujiepusha na magonjwa.
Alisema
hali hiyo ya utunzaji mazingira ya makazi yao itasaidia kupunguza hatari katika
maeneo yao.
“Kufunika
vyakula na kusafisha maeneo kwa kutunza vyoo na mazingira ya kufanyia biashara katika
hali ya usafi kutaepusha magonjwa hayo,” alisema Lyaniva.
0 comments:
Post a Comment