Mwandishi Wetu
Dk.Rehema Nchimbi |
MKUU wa Mkoa wa
Singida, Dk.Rehema Nchimbi, ameagiza Askari Kikosi cha Usalama Barabarani
kupanda miti ya matunda ili waweze kutumia matunda kwa ajili ya kuimarisha uono
wao kwa ajili ya kutekeleza vizuri majukumu yao wakati wote wanapokuwa
barabarani.
Dk. Nchimbi
ametoa agizo hilo hivi karibuni wakati akizungumza kwenye kilele
cha maadhimisho ya Wiki ya Maji yaliyofanyika kwenye Kijiji cha Iguguno Wilaya
ya Mkalama.
Alisema kiungo
muhimu kwa askari wa usalama barabarani ni macho yenye uwezo wa kuona vizuri na
kwa umbali wowote.
"Yapo
matukio yametokea askari wa usalama barabarani anajitokeza barabarani
anasimamisha gari la kiongozi,akitambua kuwa amesimamisha kiongozi,anaomba
msamaha. Anajitetea kuwa hakujua kuwa gari husika limebeba kiongozi. Unamuuliza
hata kama hukufahamu gari lina kiongozi, je hata bendera
hujaiona?",alisema.
Dk. Nchimbi
alisema kuwa askari wa aina hiyo ni wale ambao afya ya macho yao, imeathirika
na kitendo cha kutokula matunda ya kutosha.
Akisisitiza, alisema
ataanzia kukagua upandaji wa miti ya matunda kwa askari wa usalama
barabarani,kisha baadae kwa askari wote,wakuu wa wilaya,viongozi wote wa
serikali na wananchi kwa ujumla.
"Nitumie
fursa hii kuwahimiza viongozi wa madhehebu ya dini,kuwahimiza kila kaya ya
muumini kushiriki kikamilifu 'operation' panda miti miwili ya miembe.Pia
wakemee kiburi cha baadhi ya watu wanaoharibu mazingira kwa makusudi," alisema.
0 comments:
Post a Comment