Hussein Ndumbikile
Nape Nnauye |
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ameunda
kamati ya watu watano kuchunguza kitendo kilichofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar
es Salaam, Paul Makonda cha kuvamia ofisi za Clouds Media Group (CMG) Ijumaa
usiku.
Kamati hiyo imeundwa baada ya Waziri Nape kufanya ziara jana CMG
na kuzungumza na uongozi wa chombo hicho cha habari baada ya Mkuu wa Mkoa huyo
kufanya kitendo hicho akiwa na askari wenye silaha.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini wa wizara hiyo, Zawadi Msalla, Kamati hiyo itaongozwa na Mkurugenzi
wa Idara ya Habari, MAELEZO, Dk Hassan Abbas.
Wajumbe wengine ni Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri
Tanzania (TEF), Deodatus Balile, Mhariri wa Nipashe, Jesse Kwayu, Nengida
Johannes wa Wapo Radio na Mabel Masasi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
(TCRA).
Taarifa hiyo ilisema Kamati hiyo itafanya uchunguzi wa kina ili
kujiridhisha kutoka pande zote ambapo Wizara itasema hatua itakazochukua.
Wiki iliyopita, Mkuu wa Mkoa huyo kupitia picha za mitandao ya
kijamii, alionekana akivamia ofisi za kituo hicho cha habari akiwa na askari
hali iliyoleta sintofahamu kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment