Lulu Mussa, Kilimanjaro
ZIWA
Jipe liko hatarini kutoweka ikiwa hatua za haraka hazitachukuliwa kulinusuru.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, January Makamba alibainisha hayo alipofanya
ziara ya kukagua ziwa hilo ambalo sehemu kubwa imezungukwa na magugu maji.
Waziri
Makamba amesema ni lazima kuwepo mpango wa muda mfupi na muda mrefu kulinusuru
na kwamba kupitia Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamiza wa Mazingira (NEMC)
ameazimia kutangaza kuwa eneo hilo ni nyeti kimazingira.
"Tutatanga
eneo hili kuwa eneo nyeti kimazingira na tutaweka masharti ya matumizi yake,"
alisema Makamba.
Waziri
Makamba amesisitiza kuwa ni vema kunusuru ziwa hilo sasa maana ndani ya miongo
2-3 huenda ziwa hilo likatoweka
Alifafanua
kwamba kutangaza kuwa eneo hilo kuwa nyeti kimazingira itasaidi katika kuandika
maandiko mbalimbali ya miradi na kupata fedha kutoka kwa wadau na washirika wa
maendeleo ili kulinusuru.
Makamba
alisema ziwa hilo pia litawekwa chini ya uangalizi maalumu na kuweka masharti
ya matumizi bora ya eneo hilo.
"Bila
hifadhi ya mazingira hakuna maisha, na ukiyaharibu mazingira hakuna msamaha
yatakuadhibu tu," alisema na kuongeza:
“Shughuli
zozote za maendeleo iwe uvuvi, kilimo, utalii, mifugo kwa namna moja ama nyingine
zinategema hifadhi endelevu ya mazingira.”
Katika
hatua za muda mrefu Waziri Makamba amewataka wasimamizi wa Bonde la Pangani, Wizaya
ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki na Ofisi ya Makamu wa Rais kupitia Baraza la Taifa la
Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kukutana mara moja kuandaa mpango na
mtazamo wa pamoja wa kunusuru Ziwa Jipe.
0 comments:
Post a Comment