![]() |
Jaji Mutungi |
MSAJILI wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi
amezuiwa na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kutoa fedha za ruzuku kwa
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba na wenzake.
Amri hiyo ilitolewa jana na Jaji Wilfred Dyansobela baada
ya jopo la mawakili wanaowakilisha Bodi ya Wadhamini ya CUF, kuwasilisha maombi
ya kutaka kuzuiwa kwa fedha hizo kwani zilizotolewa awali, Sh milioni 369, haijulikani
zilivyotumika.
Mawakili waliowasilisha ombi hilo ni Juma Nassor, Daimu
Halfani na Hashim Mziray wakiiomba Mahakama kuzuia kutolewa fedha zingine hadi
shauri namba 21/2017 dhidi ya Msajili na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George
Masaju ya kutoa fedha hizo kwa njia za wizi hadi litakaposikilizwa na kutolewa
uamuzi.
Mawakili hao walisema fedha hizo hazikuwa kwenye mikono
salama wala hakukuwa na udhibiti wowote CUF ikizingatiwa kuwa Profesa Lipumba
alishavuliwa uanachama.
Wakili Nassor aliyewasilisha maombi hayo, alisisitiza kuwa
kwa mazingira yaliyopo ni vema na busara kwa fedha za umma zilizopaswa kutolewa
kama ruzuku kwa CUF sasa ziendelee kubaki serikalini.
Pia mawakili hao katika shauri hilo, waliiomba Mahakama amri
hiyo pia ifungamane na kesi ya msingi namba 23/2016 ya kuhoji uamuzi wa Msajili
kumtambua Lipumba kwa nafasi ya uenyekiti, ambayo kwa sasa kesi hiyo imekatiwa
rufaa/maombi ya kufanyiwa marejeo.
0 comments:
Post a Comment