Salha Mohamed
SHIRIKA la
Reli Tanzania (TRL) limezindua treni mpya ya mizigo itakayofanya safari zake
Afrika Mashariki.
Uzinduzi huo
ulifanyika Dar es Salaam jana ambapo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo,
Shaban Kiko alisema treni hiyo yenye mabehewa 20 ilianza safari kwa kupeleka
mizigo Burundi.
Kiko alisema
TRL awali haikuwa na treni kubwa kama hiyo, hivyo wananchi watarajie
kusafirisha mizigo kwa wakati na bei nafuu.
Aliongeza kuwa
huduma hiyo imezinduliwa kwa wafanyabiashara na kampuni binafsi zenye shehena
kubwa za mizigo zinazotosheleza mabehewa yote 20 ili kurahisisha kusafirisha
mizigo moja kwa moja.
"Treni hii
inayoanza safari zake leo (jana) imechukua mizigo kutoka bandari ya Dar es
Salaam, iliyotoka China na kuipeleka Burundi," alisema Kiko.
Alifafanua
kuwa treni hiyo itabeba malighafi ya chuma, mzigo unaosafirishwa na kampuni ya UBUCOM
ya Burundi.
Alisema walitoa
dola 3,056 za Marekani kwa behewa moja la mizigo ya kawaida na dola 3,024 kwa
mizigo iliyofungwa kwenye kontena.
Aidha, safari
hiyo itachukua siku mbili kuwasili Kigoma na siku moja Bujumbura huku shirika
hilo likitajwa kupunguza gharama za usafirishaji wa mizigo ya kawaida na
inayohifadhiwa kwenye kontena.
0 comments:
Post a Comment