Dalila Sharif
MADEREVA
wa daladala zinazofanya safari za Temeke na Muhimbili wameliomba Jeshi la Polisi
Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Temeke kuwaokoa dhidi ya unyanyasaji
wanaofanyiwa na baadhi ya askari wa kikosi hicho wilayani humo.
Wakizungumza
na mwandishi wa habari hizi Dar es Salaam katika barabara ya Kivungo, mtaa wa
Kitunda juzi, madereva na makondakta wao walisema wamechoshwa na unyanyasaji wa
baadhi ya askari hao, unaorudisha nyuma maendeleo yao.
Mmoja wa
madereva, Awadhi Khalifa alisema baadhi ya askari wamekuwa wakiwabambikizia
makosa na kuwanyanyasa wanapokuwa kazini na kutaka Jeshi hilo lirekebishe hali
hiyo.
“Tunakamatwa
ovyo bila makosa kila siku. Kuna makosa ya ukweli tunajua, lakini mengi ni ya
kubambikiwa. Unasingiziwa umefanya kosa hili, tena unaulizwa uandikiwe au ulipe
pesa mkononi kwa askari. Hali hiyo tumechoka nayo kwani inaturudisha nyuma
katika kazi zetu,” alisema Khalifa.
Akiunga
mkono hauli ya mwenzake, Michael Tumaa alisema wamekuwa wakiwachumia pesa
askari hao kwani wao hawafaidiki na kazi hiyo.
Alisema:
“Kituo cha daladala Chang’ombe husimamishwa na baadhi ya askari hao na kukamatwa
kwa kuonekana kuwa eti tumeiba njia, hali ambayo si kweli. Hapo hutozwa faini
au wengine kupelekwa kituo cha Polisi,” alisema Tumaa.
Madereva
hao walisema ni vema polisi wakazingatia haki katika kazi zao na kuepuka
unyanyasaji wa madereva wilayani humo.
“Rushwa
pia imetawala kwa baadhi ya polisi, tunahimiza wabadilike na wakubwa wao
wafuatilie suala hili,” alisema.
0 comments:
Post a Comment