CCM yaunga mkono hotuba ya Magufuli



CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimepongeza hotuba ya Rais John Magufuli aliyotoa kwe­nye ziara yake visiwani humo kwani ameonesha ana dhamira ya kuharakisha maendeleo ya wananchi bila kujali tofauti za kisiasa.

Akizungumza mjini humo jana, Katibu wa Kamati Maal­umu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Waride Bakari Jabu, alisema CCM inaunga mkono na kupongeza hotuba zilizotolewa na Rais Magufuli huko Unguja na Pemba kwa kusisitiza dhamira ya Serikali zote mbili kuwaletea wananchi maendeleo.

Waride alisema viongozi wa chama chake na wananchi kwa wote sasa wanatakiwa kushiriki­ana katika ujenzi wa maendeleo ya Taifa ili Zanzibar iweze kufikia uchumi mkubwa katika nchi za Afrika.

“Ziara ya Rais Magufuli im­etoa mwongozo imara wa kuwa­kumbusha watendaji na vion­gozi nchini juu ya dhamana na mambo ya msingi wanayotakiwa kuyatekeleza kwa wananchi,” alisema

Alifafanua kuwa,”CCM tu­naunga mkono kwa nguvu zote hotuba ya Rais Magufuli kwani imezungumzia na kugusia mam­bo ya msingi yanayogusa maisha ya wananchi, hasa wa kipato cha chini na kutoa mwongozo wa namna Serikali zinavyoendelea na mikakati imara ya kuimarisha uchumi na maendeleo ya Taifa kwa jumla.

“Pia tunatakiwa kuendelea kuwa wamoja na wazalendo bila ya kujali tofauti zetu za kidini, kisiasa na kikabila kwa kulinda amani na utulivu wa nchi zetu kwani ndiyo siri ya mafanikio ya nchi zetu”. Katibu huyo alisema Dk. Magufuli ameonesha nia ya dhati ya kuendelea kutafuta fursa mbalimbali za miradi ya maen­deleo itakayoweza kuharakisha maendeleo ya Zanzibar.

Alisema miongozo mwa mam­bo ya msingi yaliyosisitizwa na Dk. Magufuli pia yanaungwa mkono na CCM Zanzibar ni dhamira ya kuhakikisha Zanzi­bar inakuwa ni nchi ya viwanda vya kusindika samaki wanaoto­kana na uvuvi wa kisasa wa ba­hari kuu vitakavyotoa fursa za ajira kwa vijana na wananchi.

Waride alipongeza juhudi zina­zofanywa na Serikali ya Muun­gano wa Tanzania kwa kufungua milango ya wawekezaji wakubwa kuwekeza Zanzibar huku waki­tafuta wahisani kutoa mamilioni ya fedha za kuendesha miradi ya kijamii ukiwemo mradi wa maji safi Unguja uliotolewa fedha za mkopo na Serikali ya India.

Alisema kwa ushirikiano wa Rais Dk. Magufuli na Dk. Shein, CCM inaamini kwamba Tanza­nia bara na Zanzibar kwa ujumla zitakuwa nchi za kupigiwa mfa­no duniani katika nyanja mbal­imbali za kimaendeleo, kisiasa na kijamii.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo