Zijue dalili, tiba ya tezidume



MWANAMUME anayehisi kwenda haja ndogo mara kwa mara au kushindwa kuimaliza, anapaswa kuchunguzwa ili kujua kama anaugonjwa wa tezidume.

Daktari wa Magonjwa ya Binadamu, Dk Stephen Kisaka amesema mwenye tezidume asipotibiwa mapema, anaweza kupata matatizo ya kiafya kama ya figo, kibofu cha mkojo na shinikizo la damu.

Matatizo mengine, alisema ni kushindwa kutoa mbegu za kiume wakati wa tendo la ndoa, damu kuganda, maambukizi ndani ya njia ya mkojo na homa ya mapafu. Dk Kisaka alisema ugonjwa huo ukibainika mapema ni rahisi kuutibu au kuudhibiti.

Hata hivyo, alisema watu wengi huchelewa kwenda hospitali na matokeo yake hujikuta wakiathirika
kiafya, kwa sababu wakati huo tiba inachukua muda mrefu au kulazimika kufanyiwa upasuaji. Katika maelezo yake, Dk Kisaka alieleza namna ya kujikinga na mambo ambayo mwanamume anapaswa kuepuka ili asipate tatizo hilo.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo