Mbunge amgeukia Rais Magufuli


Rais John Magufuli
KAULI ya Rais John Magufuli kutaka Watanzania kufanya kazi na kuacha kudai kuwa fedha zimekauka mifukoni tangu alipoingia madarakani, jana ilipingwa na Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga (CCM) aliyemtaka kiongozi huyo kubadili aina ya uongozi wake akieleza kwamba Watanzania wanakabiliwa na maisha magumu.

Mbunge huyo ambaye husifika kwa kauli tata bungeni, alisema hayo juzi wakati akichangia mjadala wa Muswada wa Sheria ya Upatikanaji Taarifa mwaka 2016, iliyowasilishwa kwa mara ya pili bungeni juzi na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe.

“Leo naanzia nyumbani. Mimi ni mbunge kijana na nawakilisha vijana ambao wengi wao sasa wanaishi maisha magumu,” alisema kwa upole.

“Hali ya maisha ni ngumu sana, namwomba Rais hapo alipopashika apaachie kwa sababu si mahali pake,” alisema.

Mara kadhaa Rais Magufuli amekuwa akitaka wananchi kufanya kazi, kubainisha kuwa katika utawala wake ni ngumu kupata fedha kama hufanyi kazi.

Mara ya mwisho kiongozi mkuu huyo wa nchi kutoa kauli hiyo ilikuwa wiki iliyopita katika mkutano wa 14 wa mwaka wa wahandisi uliofanyika Dar es Salaam, ambapo alisema kipindi cha nyuma fedha zilikuwa nyingi kwa sababu baadhi ya watu walikuwa wakiiba fedha za Serikali, ila kwa sasa jambo hilo limedhibitiwa.

“Fedha za bure hazipo na ndiyo maana thamani ya nchi na fedha yetu imeanza kuongezeka na mfumuko wa bei sasa umeshuka mpaka asilimia 5.1,” alisema Rais Magufuli katika mkutano huo.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo