Chumvi itumiwe kwa uangalifu kuzuia magonjwa


WATAALAMU wa afya wameshauri kuwa chumvi ni lazima itumike kwa uangalifu ili kuepuka madhara ya kiafya yanayoweza kumpata mlaji.       

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dk. Phili Chilo, alisema chumvi ikitumiwa vibaya husababisha maradhi ya shinikizo la damu na magonjwa ya moyo.

Alisema wastani wa kiwango cha chumvi unaokubalika kiafya mtu anatakiwa kula kwa siku nzima ni miligramu 2300 tu, sawa na kijiko kidogo cha chumvi. Kwa wale wanaosumbuliwa na maradhi ya moyo na shinikizo la damu wanatakiwa kutozidisha kiasi cha miligramu 1,500 ya chumvi kwa siku.

Wapo wanaopinga kipimo hicho wanaodai kuwa, watu wanatokwa sana na jasho, wanaofanya kazi za sulubu, wanamichezo na wanaoishi katika nchi za joto wanatakiwa kula chumvi zaidi.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo