Askari JWTZ apigwa risasi, aporwa mamilioni


Abraham Ntambara

MKAZI wa Tabata Kimanga, Dar es Salaam, anayedhaniwa kuwa askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), amepigwa risasi na wanaoaminika kuwa majambazi na kumpora Sh milioni 5. Tukio hilo lilitokea jana Tabata Kimanga karibu na kituo cha daladala Jiandae, ambako watu hao wakiwa na pikipiki aina ya Boxer, walimvamia Richard Halfani aliyekuwa akijiandaa kuingia nyumbani kwake na kumpiga risasi.

Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ ) Kanali Ngemela
Lubinga alipoulizwa alisema: “Sina taarifa za tukio hilo na siwezi kulizungumzia kwa kuwa niko Mwanza kikazi, naomba uwasiliane na makao makuu.”

Hata hivyo, wahusika Makao Makuu ya JWTZ walipotafutwa hawakupatikana. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ilala, Salum Hamdun (pichani chini) alithibitisha tukio hilo akisema: “Mtu anayesadikiwa kuwa ni askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania anayeitwa Richard Suleimani Halfan ndiye aliyevamiwa na majambazi.”

Kamanda Hamdun alisema majambazi hao walimjeruhi Halfan kwa risasi na kumnyang’anya kiasi cha fedha alichokuwa nacho. Alifafanua, kwamba taarifa za awali zinaonesha kuwa askari huyo alikuwa amekwendabenki na wakati akirudi watu walimfuatilia na alipofika maeneo hayo ambayo pia ni jirani na nyumbani kwake, alivamiwa.

Alisema baada ya kujeruhiwa, alikimbizwa kwenye hospitali ya Amana kwa matibabu. Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, alisema tukio hilo lilitokea jirani na nyumba ya wageni ya Emirates ambapo askari huyo alikuwa amekaribia lango la nyumba yake.

Alisema askari huyo alipigwa risasi na kuporwa fedha alizokuwa alizohifadhi kwenye bahasha kubwa ya khaki na baada ya tukio hilo, alipiga kelele za kuomba msaada, ndipo watu walijitokeza kumsaidia.

Alisema muda mfupi kabla ya uhalifu huo kutokea, askari walifika eneo hilo na kuokota waliokota baadhi ya vielelezo yakiwamo maganda ya risasi kwa ajili ya uchunguzi.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo