Zungu amwomba radhi Mbowe


Fidelis Butahe, Dodoma

Freeman Mbowe
MWENYEKITI wa Bunge, Musa Azan Zungu amemwomba radhi Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe kwa kushindwa kutambua mchango wake kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.

Zungu ambaye ni Mbunge wa Ilala na Mwenyekiti wa Bunge, alitoa kauli hiyo jana bungeni baada ya kubanwa na wabunge wa Chadema, Mwita Waitara (Ukonga) na Pascal Haonga (Mbozi), ambao waliomba Mwongozo wakihoji sababu za Mwenyekiti huyo kutaja watu waliotoa msaada wa waathirika hao na kushindwa kumtaja Mbowe.

“Nikubali sikumtaja na nimwombe radhi kwa sababu alihusika. Hili suala lisitugawe litufanye tuwe kitu kimoja,” alisema Zungu baada ya kusikiliza hoja za wabunge hao.

Katika Mwongozo wa kwanza, Waitara alisema Zungu wakati akitaja waliotoa msaada na kufika eneo la tukio kuwajulia hali waathirika wa tetemeko hilo, alimtaja Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati akitambua wazi kuwa baada ya kiongozi huyo wa shughuli za Serikali bungeni kuondoka, Mbowe alikwenda mkoani humo kutoa msaada.

“Sisi wabunge wa upinzani tumechangisha fedha na kumkabidhi kiongozi wa upinzani azifikishe sehemu husika ili kusaidia waliopata maafa haya. Naomba Mwongozo wako tunapopongezana na wewe humtaji kiongozi mkubwa wa upinzani maana yake nini?” Alihoji Waitara.

“Si jambo jema, pia kumekuwa na malalamiko ya kutotambuliwa kwa mameya na wabunge wa upinzani wanaohudhuria matukio ya kitaifa.”

Haonga naye aliomba Mwongozo kama huo, kubainisha kuwa kitendo hicho ni dharau kwa kiongozi huyo wa upinzani bungeni.

Awali Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini (Chadema) aliomba Mwongozo juu ya wabunge kutuhumiwa kuhongwa fedha baada ya gazeti la kila sikumnukuu Mbunge wa Manonga (CCM), Seif Gulamali, akisema wabunge wanahongwa ili kutetea hoja bungeni.

Katika Mwongozo huo, Selasini alisema jambo hilo likiachwa linaingilia Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge na kumtaka Mbunge huyo kuwataja kwa majina wahusika ili kuondoa dhana ya wabunge wote kuhusishwa na jambo hilo.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo