Uongo unaugharimu ubongo


William Shao
KWA muda mrefu, ilikuwa inaaminika kuwa kusema uongo kunamtesa sana yule anayeusema uongo huo kiasi kwamba baadhi ya wataalamu wanasema ukiwa mwongo, basi uwe na kumbukumbu ya kile ulichosema.

Hii peke yake inamaanisha kuwa ukisema uongo lazima uupe ubongo wako kazi kubwa ya kuweka kumbukumbu ya yale uliyoyasema, tofauti na mtu anayesema kweli.

Watafiti katika Chuo Kikuu cha Pennsylvania nchini Marekani wamegundua kuwa ubongo unalazimika kufanya kazi kubwa na kwa bidii zaidi unaposema uongo kuliko unaposema ukweli.

Profesa Mtafiti wa Magonjwa ya Akili na Mtafiti wa Masuala ya Sayansi katika Chuo Kikuu cha Pennsylvania, Dk Daniel Langleben, amekuwa akilifanyia utafiti jambo hilo kwa miaka kadhaa kwa kutumia mashine ya fMRI (magnetic resonance imaging) kubaini ni sehemu gani za ubongo zinazochochewa wakati mtu anaposema uongo.

Aligundua kuwa wakati tusemapo uongo, ubongo unahitaji kwanza kuanza kazi ya uchakataji. Kisha, “Kwa kutumia silika, kwanza mtu mwongo ataanza kufikiria jawabu la kweli kabla hajafikiria kuongea uongo,” linaandika gazeti The News la Mexico City.

“Katika ubongo huwezi kupata kitu cha bure. Mchakato wa ubongo wa kusema uongo ni mgumu zaidi kuliko mchakato wa ubongo wa kusema ukweli, na unasababisha matumizi makubwa zaidi ya nyuroni (seli za neva),” anasema Dk Langleben.

Ongezeko la ziada la matumizi ya nyuroni katika ubongo yalionekana katika mashine ya fMRI kama glopu ya umeme. “Hata kwa mtu ambaye hasemi uongo sana, uongo bado ni kazi ngumu kwa ubongo wake,” likaandika gazeti hilo.

Hata hivyo, Taasisi ya Kisayansi ya Marekani, katika jarida Scientific American Mind la Septemba 2011, iliandika: “Kwanza unalazimika kutunga hadithi (ya uongo), pili utalazimika kuukumbukautunzi wako na tatu utalazimika kuhakikisha unaaminika kazi ambazo zinahitaji matumizi makubwa ya ubongo.”

Aidha, mwandishi Mmarekani, Mark Twain (1835-1910), katika kitabu Adventures of Huckleberry Finn © 1884, aliandika: “Ukisema kweli huna haja ya kukumbuka chochote.” Kwa maana hiyo, mwongo anaupa ubongo wake mzigo mkubwa kuliko ilivyofikiriwa awali.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo