Trafiki kutoa namba kupiga simu bure


MKUU wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Mohamed Mpinga amesema wanafikiria kutoa namba ya simu itakayom­wezesha abiria kupiga bure, ikiwa ni njia itakayorahisisha utoaji wa taarifa za madereva wanaovunja sheria za bara­barani.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Kamanda Mp­inga alisema baadhi ya abiria hushindwa kutoa taarifa za madereva wanaokiuka sheria za usalama barabarani kwa kisingizio cha kukosa fedha za kupiga simu.

Kamanda Mpinga alisema kuwa, kutokana na ma­dai hayo ya wananchi, wameamua kuweka namba hizo za kupiga bure ili ziweze kusaidia kupunguza ajali.

“Katika utoaji wa taarifa kumekuwa na changamoto ya baadhi ya abiria kushind­wa kupiga simu na kutoa taarifa za madereva wanao­vunja sheria kwa kisingizio kuwa, hawana fedha kwenye simu zao,” alisema Mpinga.

Alisema tangu kuanza ku­toa elimu kwa abiria ya kuo­na umuhimu wa usalama barabarani na kubandika namba za simu kwa ajili ya kutoa taarifa za madereva wanaoendesha magari kwa mwendo wa kasi kume­kuwa na mwitikio mkubwa wa kupiga simu na kuripoti matukio hayo.

Aliongeza kuwa hata madereva wa ma­basi na malori pia wameha­masika katika kujali sheria za barabarani na wameanza kulindana wenyewe kwa we­nyewe, ambapo huelezana na hata kuripoti sehemu husika ili wachukuliwe hatua za kishe­ria.

Mpinga alisema baadhi ya abiria hawajui umuhimu wa kuripoti matukio hayo, ambapo wamekuwa wak­ichangia kukwamisha kazi hiyo, hivyo wamekuwa wak­iwasakama abiria wanaotoa taarifa na kuwavunja moyo wa kufanya hivyo.

“Wakati mwingine kuna abiria ambao hushabikia mwendo kasi, wanapoona wenzao wakitoa taarifa hu­wasakama na kuwaambia washuke,”alisema.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo