Uingereza ndilo taifa lenye wabinafsi wengi duniani


William Shao
KWA mujibu wa utafiti mmoja, Waingereza ndio watu wenye ubinafsi zaidi duniani, ndiyo jamii inayokazia zaidi faida za kibinafsi kuliko watu wa nchi nyingine yoyote duniani, limeripoti gazeti la Daily Telegraph la nchini Uingereza.

Uchunguzi mwingine ulionesha kwamba Waingereza wanapatwa na huzuni na mifadhaiko kuliko raia wa taifa jingine lolote duniani. Wataalamu wanaamini kuwa mambo hayo mawili ubinafsi na huzuni yanahusiana.

Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Northwestern kilichoko Chicago, Marekani, ulilinganisha jamii mbalimbali duniani, kama zile zinazopatikana katika nchi za Ulaya na zile za China na Taiwan.

Ilionekana kwamba kwa kuwa jamii za China na Taiwan zinathamini zaidi ushirikiano katika jamii badala ya ubinafsi, watu wanalindwa wasipatwe na matatizo ya akili.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na mwanasaikolojia wa Uholanzi, Geert Hofstede, imegundulika kuwa katika nchi zilizo na jamii zenye watu wabinafsi zaidi, Uingereza ilishika namba moja katika orodha, ikifuatiwa na Marekani, Australia na nchi nyingine za Magharibi. Katika nchi za Ulaya, “jamii yenye ubinafsi inatufanya tuhuzunike,” linaripoti gazeti Telegraph.

Hata hivyo, kiwango cha huzuni na mfadhaiko katika jamii hizo ni cha juu sana kuliko mahali pengine popote duniani, kwa mujibu wa utafiti wa Shirika la Afya Duniani (WHO) uliojulikana kama ‘Depression: A Global Public Health Concern’.

“Tumegundua uhusiano wa ajabu sana kati ya ubinafsi, huzuni na mfadhaiko,” anasema Dk. Joan Chiao, mwandishi wa taarifa ya utafiti huo, na kuongeza, “Mataifa yenye watu walio na ubinafsi zaidi wameonesha kiwango cha juu sana cha huzuni na mfadhaiko.”

“Kiasi cha mmoja kati ya watu 10 nchini Uingereza anateswa na ama huzuni au mfadhaiko ikilinganishwa na mmoja kati ya watu 12 katika Bara la Ulaya,” liliandika pia gazeti la Telegraph na kuongeza: “Inakadiriwa kuwa kiwango cha mfadhaiko na huzuni nchini China ni kiasi cha mmoja kati ya watu 25.”

Huenda wengine wakadhani kuwa ubinafsi huo umechochewa na uzalendo wa Waingereza kwa nchi yao. Lakini kama ndivyo, kamusi moja inafafanua uzalendo kuwa “kutukuza taifa moja juu ya mataifa mengine yote na kusisitiza kuendelezwa kwa utamaduni wake na maslahi ya taifa hilo badala ya mataifa mengine.”

Mtafiti Ivo Duchacek, ambaye ni profesa wa siasa, alisema katika kitabu chake, Conflict and Cooperation Among Nations: “Uzalendo hugawanya wanadamu katika visehemu visivyoweza kuvumiliana. Kwa sababu hiyo, watu hujiona kuwa Wamarekani, Warusi, Wachina, Wamisri, Waperu, au watu wa taifa lingine, kisha wanajiona kuwa wanadamu ikiwa kwa vyovyote wao hujifikiria hivyo.”

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa aliandika hivi: “Matatizo mengi tunayokabili leo ni kwa sababu ya, au yanatokana na mitazamo isiyofaa ambayo tumeisitawisha, mengine bila kujua. Mawazo hayo yanajumuisha wazo la kwamba ‘nitaitetea nchi yangu iwe imekosea au la.”

0754/0655-989837
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo