Vyeti bandia vyatimua 11 Muhimbili


Salha Mohamed

HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MNH), imewasimamisha kazi wafanyakazi 31 baada y  kubainika wakitumia vyeti bandia huku wengine 48 wakitiliwa shaka uhalali wa vyeti vyao.

Tayari watumishi hao wameondolewa kwenye mfumo wa kumbukumbu za kiutumishi na mishahara, baada ya uhakiki huo kukamilika.

Uhakiki huo unaofanywa na Baraza la Taifa la Mitihani (NACTE) umekuja ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Serikali kutambua na kuondoa watumishi hewa na wasiokuwa na sifa kwenye nafasi mbalimbali nchini.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma MNH, Aminiel Aligaesha alisema wafanyakazi waliosimamishwa, 11 ni wauguzi, watatu wahudumu wa afya, wahasibu wawili, watunza kumbukumbu za afya ya wagonjwa watano, makatibu muhtasi wawili, wafanyakazi wa maabara watatu, mfamasia, karani wa masjala, fundimchundo, dobi na Ofisa Ustawi wa Jamii.

“Muhimbili inaendelea na uhakiki wa vyeti vya wafanyakazi kupitia NECTA ambapo hadi sasa tayari wafanyakazi 1,600 wamehakikiwa vyeti vya kidato cha nne kati ya wafanyakazi 3,000 waliopo,” alisema.

Alisema katika mchakato wa uhakiki wa wafanyakazi hospitalini hapo bado wafanyakazi 1,400 hawajahakikiwa na kwamba wanaendelea kuhakikiwa. Alisema watumishi waliosimamishwa wamewaandikia barua za kujieleza kila mmoja ndani ya siku 14 kwa mujibu wa kanuni na taratibu za utumishi wa umma, ili kuwapa nafasi ya kujitetea kabla ya hatua stahiki.

“Tumebaini kuwa wafanyakazi 48 vyeti vyao vinatia shaka uhalali wao hivyo tumewaandikia barua ili kuleta vyeti halisi ili kuchunguzwa zaidi na Mamlaka husika,” alisema.

Alisema kati ya 48 wafanyakazi 23 ndiyo walioleta vyeti na ambavyo tumevipeleka NACTE ambapo sasa wanasubiri waliobaki 25 wapeleke.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo