Asilimia 95 wananchi wataka Serikali akosolewe



 Abraham Mtambara

ASILIMIA 95 ya wananchi wanaunga mkono ukosoaji Serikalihuku wananchi saba kati ya 10 wakisema demokrasia ndio mfumo bora wa utawala.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti ya Twaweza, Aidan Eyakuze alibainisha hayo jana Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa ripoti ya utafiti uliofanywa na taasisi hiyo kuhusu demokrasia, udikteta na maandamano nchini.

“Matokeo haya yanatokana na takwimu zilizokusanywa kutoka kwa wahojiwa 1,602 kati ya Agosti 23 na 29,” alisema Eyakuze.

Eyakuze alisema asilimia 69 wanakubali kuwa demokrasia ni mfumo bora wa utawala ingawa baadhi ya wananchi wanasema kwa kiwango fulani utawala usio na demokrasia unaweza kukubalika. Aliongeza kuwa pamoja na kukubalika kwa Serikali ya kidemokrasia, wananchi walikuwa na maoni tofauti kuhusu majukumu ya vyama vya upinzani.

Alisema katika utafiti huo, asilimia 86 ya waliohojiwa walisema Tanzania inahitaji vyama vingi vya siasa, ili kuwapa fursa ya kuchagua kiongozi anayefaa kuwaongoza, huku asilimia 80 wakisema baada ya uchaguzi vyama vya upinzani vinapaswa vikubali kushindwa na visaidiane na Serikali kujenga nchi.

Alifafanua kuwa asilimia 20 tu ndio walisema wapinzani waifuatilie na kuiwajibisha Serikali, wakati asilimia 49 wakisema mikutano baada ya kampeni hukwamisha maendeleo.

“Asilimia 47 walisema upinzani uruhusiwe kufanya mikutano yao bila pingamizi,” alisema.

Alifanya asilimia 60 ya wananchi walikubaliana na kuzuiwa kwa mikutano ya vyama vya siasa, ambapo asilimia 70 ya wafuasi ni wa chama tawala na 33 ya wa vyama vya upinzani, huku kwa upande wa ushiriki wa maandamano asilimia 50 hawakuwa tayari ingawa asilimia 29 walikuwa tayari.

Eyakuze alisema ndani ya miezi michache, baada ya kuanzishwa kwa harakati za UKUTA na kufahamika kwa wananchi asilimia 16, kati yao alisema asilimia 55 walio karibu na vyama vya upinzani waliunga mkono, huku asilimia 44 wakipinga wakati asilimia ndogo ambayo ni sita kutoka chama tawala wakiunga mkono pia.

Aidha, aliongeza kuwa asilimia 11 ya wananchi waliamini kuwa Tanzania inaongozwa kidikteta, huku asilimia 58 wakipinga uwepo wa utawala huo nchini. Msemaji wa CCM, Christopher ole Sendeka akitoa maoni yake juu ya utafiti huo, aliuunga mkono na kusema utawala wa Rais John Magufuli si wa kidikteta ila unafuata kanuni, sheria na mamlaka ya kikatiba.

“Watu wanaosema kwamba utawala wa Rais Magufuli ni wa kidikteta ni waliozibiwa mianya ya ulaji, na hata wanasiasa wanapiga kelele kwa sababu wapo waliokuwa wakinufaika na mianya hiyo,” alisema Sendeka.

Alisema kuna demokrasia nchini akifafanua kuwa bila demokrasia, viongozi wa vyama vya upinzani wasingepata uhuru wa kufanya mazungumzo na waandishi wa habari na kukosoa Serikali.

Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe aliunga mkono utafiti huo na kusema ili mtu apinge, lazima naye awe amefanya utafiti ambapo pia alibainisha moja ya udhaifu wa utafiti huo.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo