Waandishi wazuiwa kushuhudia ndege


KUNDI la wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari jana lilijikuta katika hali ya sintofahamu, baada ya kuzuiwa kuingia kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), kushuhudia kuwasili kwa ndege mpya aina ya Bombadier Q400 Next- Gen, ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL).

Awali, wananchi walitakiwa kujitokeza kushuhudia ndege hiyo ikiwasili, lakini baadaye taarifa zilieleza kuwa hafla ya mapokezi yandege hiyo zimefutwa na isingewasili jana kama ilivyotangazwa.

Waandishi hao waliwasili JNIA tangu saa tano asubuhi kwa ajili ya mapokezi hayo, lakini hawakupata ushirikiano kutoka kwa maofisa wa Wizara ya Uchukuzi na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), ambao walitupiana mpira wa kuhusika kutoa taarifa sahihi na ruhusa ya kwenda kushuhudia kuwasili
kwa ndege hiyo.

Miongoni mwa vyombo vya habari vilivyokumbwa na adha hiyo mbali na gazeti hili ni BBC, ITV, Azam TV, Chanel Ten, Ayo TV, ZBC, TBC, Mwananchi, JAMBO LEO, Mtanzania na Radio France (RFA).

Hadi waandishi wetu wanaondoka uwanja wa ndege wa zamani (Terminal I) saa nane mchana, hawakufanikiwa kuingia uwanjani kushuhudia ndege hiyo.

Yawasili

Hata hivyo, baadaye Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa alitoa taarifa kwa vyombo vya habari za kuwasili kwa ndege hiyo mpya ya kwanza iliyonunuliwa na Serikali kwa ajili ya kutumiwa na ATCL, iliyotua jijini ikitokea Canada ilikotengenezwa.

Kwa mujibu wa Msigwa, ndege hiyo aina ya Bombadier Q400 NextGen ilitua saa 6:15 mchana, kisha kupewa heshima maalumu, ambayo hutolewa kwa ndege mpya inayotua nchini mwake.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo