Kauli za Magufuli zakoleza mpasuko Zanzibar



KAULI ya Rais John Magufuli kwamba Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein hapaswi kushirikiana na wapinzani, hasa Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hammad imepokewa kwa hisia tofauti, huku baadhi ya wasomi na wanasiasa wakieleza kuwa inaweza kuongeza mpasu­ko wa kisiasa visiwani humo.

Juzi wakati akihutubia kwe­nye mkutano wa hadhara wa kushukuru wananchi wa Zanzi­bar kwa kumchagua kuwa Rais katika Viwanja wa Demokrasia Unguja, Rais Magufuli alitumia muda mwingi kuzungumzia siasa za Zanzibar na kuwaponda wapinzani, kikiwamo kitendo cha Maalim Seif kumnyima mkono Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein.

“Juzi wote tulishuhudia msiba­ni na Watanzania wameona kwenye picha, Dk Shein kwa unyenyekevu alimsalimu mtu fulani, lakini akakataa. Mkono huohuo ambao ameukataa, ndi­yo Rais Shein anautumia kusaini fedha za safari na matibabu.” alisema Rais Magufuli na kuen­delea;

“Kweli una moyo wa upendo, natamani ningekuwa na hata robo maana mimi nisingeweza kutumia mkono wangu kum­sainia mtu akatibiwe, wakati mkono huohuo aliukataa.”

Kuhusu wapinzani, Rais Magu­fuli alisema hawezi kumuingiza mpinzani kwenye Serikali yake kama alivyofanya Dk Shein na kufafanua kuwa ndani ya Serika­li yake, hatakuwa tayari kumuin­giza mpinzani afanye naye kazi.

Kwa nyakati tofauti jana, was­omi na wanasiasa walisema, kwa hali ilivyo Zanzibar, Rais Magu­fuli alipaswa kusaidia kuleta mwafaka katika mpasuko wa ki­siasa uliopo badala ya kutoa kau­li inayoweza kuongeza mpasuko.

CUF yatoa tamko

Kaimu Mwenyekiti wa CUF, Julius Mtatiro alisema chama hi­cho kimesikitishwa na kauli hizo za Rais alizoziita za uchochezi, kupandikiza chuki na uhasama miongoni mwa wananchi wa Zanzibar.

“Kutokana na hadhi ya taasisi yake (Urais), CUF imesikitishwa na Rais kutoa kauli za kuwagawa wananchi na kutaka kujenga chama chake kwa njia ya vitisho na kutumia vyombo vya dola,” alisema Mtatiro.

Kiongozi huyo wa CUF alise­ma kauli hiyo ya rais Magufuli ni mwendelezo wa kauli kadhaa alizowahi kutoa huku nyuma akihamasisha matumizi makub­wa ya kijeshi yasiyozingatia she­ria kwa wananchi wa Zanzibar.

“CUF haitakuwa tayari kum­wona (Rais) anaiingiza nchi katika mgawanyiko, vitisho na visasi vinavyoweza kuzaa machafuko. Ifahamike kwamba wananchi hawakumchagua kwa ajili ya kuyaandaa majeshi ya­pambane nao,” alisema.

Wasomi

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Bashiru Ali alisema viongozi wote waliopita na Rais Magufuli wanajua chan­zo cha mgogoro wa Zanzibar, lakini wanafumbia macho na kuhangaika na mambo yasiyo na msingi.

Dk Bashiru alisema viongozi hao wanajaribu kuaminisha jamii kuwa mgogoro wa Zanzi­bar ni uchaguzi jambo ambalo si kweli na kuwataka wanasiasa waache malumbano yasiyokuwa na tija katika majukwaa ya ki­siasa.

“Unajua tatizo la Zanzibar linahitaji mazungumzo na si jazba wala ukali kwani ni tatizo halisi si la kuktengeneza kama wanavyofanya wanasiasa na kuchukulia ni mtaji wa kisiasa,” alisema.

Alisema mgogoro huo usifa­nanishwe na tofauti za kisiasa kati ya CUF na CCM kwa kuwa sasa ni suala lililo kwenye jamii na kwamba Rais Magufuli ana­paswa kuchagua maneno ya ku­zungumza badala ya kutumia au kufikiria kwamba ubabe na ha­sira vinaweza kumsaidia.

Dk Bashiru alisema wapo watu wanaofikiria kuwa uchaguzi wa mwaka 2020 utakuwa suluhisho la hali ilivyo sasa lakini si kweli kwa sababu uchaguzi ni ma­tokeo ya kuendeleza hali iliyopo na siyo kutafuta ufumbuzi.

Dk. Lwaitama

Mhadhiri Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dk. Azaveli Lwaitama alisema ana­chofanya Rais Magufuli anajua faida na hasara zake, hivyo kuna uwezekano wa yeye kuangalia hali itakavyokuwa.

Dk Lwaitama alisema ni dha­hiri kuwa Rais Magufuli am­ethibitisha kwamba uchaguzi ulikuwa halali, hivyo kutaka apeleke ujumbe kuwa mgogoro wa Zanzibar siyo uchaguzi.

“Kimsingi kauli hizo ni ngu­mu kuziunga mkono hasa sisi ambao tunatambua siasa za Zan­zibar. Zinaweza kuzalisha jambo lingine ambalo halikuwepo, la­kini tusubiri matokeo kama ya­takuwa chanya au hasi,” alisema.

Lwaitama alisema marais wastaafu Alhaji Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa ndiyo wenye uwezo wa kutatua mgogoro wa Zanzibar.

Wanasiasa

Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo Anna Mghwira alisema anaamini kinachohitaji­ka Zanzibar si ubabe na kwamba kumlazimisha Rais Shein kuwa mkali si njia sahihi, kwani Wa­zanzibari wanatambua nini kili­fanyika hata kufikia hali iliyopo sasa.

“Naamini Zanzibar kuna tatizo na kama tunahitaji kutatua njia ya mazungumzo ni muhimu zaidi kuliko ubabe na vitisho,” alisema.

Mwenyekiti wa Chama Cha Kijamii (CCK), Constantine Ak­itanda alisema kauli za Rais ni za mrengo mkali ambao hau­jazoeleka nchini hivyo zinaweza kuongeza mgogoro.

Alisema kinachoonekana kwa sasa ni CCM kuendelea kupoteza nguvu Zanzibar, hivyo rais ana­paswa kutumia diplomasia bada­la ya lugha ya ukali inayoweza kuvuruga mambo.

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mjini Magharibi Zan­zibar (Chadema), Maraim Msa­baha alisema kauli hizo zina­warudisha nyuma Wazanzibar kwani hali ilishaanza kutenga­maa.

Msabaha alisema hadi sasa Pemba watu hawazikani, ha­washirikiani katika sikukuu na mambo mengi ambayo ni ya kijamii, hivyo Rais angepaswa kusoma alama za nyakati na kuwa mstari wa mbele kumaliza mgogoro huo.

Mbunge wa Jimbo la Mpen­dae (CCM) Salim Hassan Turky, alisema alichofanya Rais ni ku­tuma ujumbe kwa umma kuwa uchaguzi haupo, hivyo Wazanzi­bari wachape kazi.

Turky alisema kitendo cha Seif Sharif Hamad kukataa kumpa mkono Rais Dk. Shein mkono hakikupaswa kufumbiwa ma­cho na alichofanya Magufuli ni sahihi.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo