Vijana Chadema wapongeza ununuzi


Abraham Ntambara

BARAZA la Vijana wa Chadema (BAVICHA) limempongeza Rais John Magufuli kwa kutekeleza ahadi yake ya kununua ndege wakisema kwa teknolojia ya leo ingekuwa vyema kama angenunua ndege kubwa kuliko Bombardier Q400.

Akizungumza na JAMBO LEO jana Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Baraza hilo, Julius Mwita alimpongeza Rais Magufuli kwa kutekeleza ahadi yake hiyo.

“Kwanza nimpongeze Rais Magufuli kwa kutekeleza ahadi yake, kwani kuna viongozi wengine wemekuwa wakiahidi bila kutekeleza,” alisema Mwita.

Lakini pamoja na kupongeza, Mwita alisema kwa maendeleo ya kiteknolojia ya leo si vema kujivunia kwa kununua ndege hizo, kwa kuwa badala ya kusonga mbele “ni kama tumerudi nyuma kwa takribani miaka 50”.

Alisema ili kuendana na wakati huu wa maendeleo ya Sayansi na Teknolojia, zingenunuliwa Airbus A310 au 308 za kubeba abiria wengi ili kusaidia kwenye ushindani mkubwa wa kibiashara na mashirika mengine.

Aidha, alisema itakuwa vigumu kwa watu wenye haraka kutumia ndege hizo akitolea mfano kwamba zikitumika kwa safari ya Dar es Salaam - Mwanza ni saa 3:45 wakati Airbus inatumia saa 3:20.

Mwita aliongeza kuwa ndege hizo hazikidhi mahitaji kwa kuwa ni chache wakati nchi ni kubwa ambapo wahitaji wa usafiri huo ni wengi hivyo kwa msingi huo angesubirikununua angalau nne ili kuleta alichokiita maana zaidi kuliko sasa. Hata hivyo, akizindua ndege hizo jana, Rais Magufuli alisema Serikali itanunua ndege kubwa mbili siku za karibuni, moja ikibeba abiria 160 na nyingine 240.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo