Singeli na kasi ya 4G mnatambua inakokewnda?



KUTOKA DAWATI LA ZEZE ‘The Dream Team’


Said Mwinshehe
KUNA kila sababu ya kupongeza kazi nzuri ambazo zinafanywa na wasanii mbalimbali nchini. Wamekuwa wakifanya kazi ambazo si tu zinawatambulisha wao bali na Taifa kwa ujumla. Hongereni wasanii kwa kazi nzuri.

Baada ya utangulizi huo naomba kutumia nafasi hii kuzungumzia muziki wa singeli ambao kwa hakika umetokea kupendwa na Watanzania wengi na hasa kundi la vijana.

Ni aina ya muziki ambao umetokea kukubalika na kupendwa na walio wengi.Zipo sababu nyingi lakini kwa sehemu kubwa unaonekana ni muziki ambao umekuja kuleta ushindani dhidi ya Bongo Fleva.

Wakati muziki huo ukiendelea kupendwa kwa kasi ya 4G ni vema wadau wa muziki huo wakatambua kuwa bado wanakazi ya kufanya ili muziki huo kukubalika na makundi yote.Bado kuna dhana kuwa muziki huo ni wakihuni.

Dhana hiyo itaondolewa na wasanii wa muziki huo kwa kuonesha kuwa si muziki wa wahuni na unaweza kupendwa na mtu yoyote.

Profesa Jay kupitia wimbo wa Kazi ambao ameuimba kwa mtindo wa singeli ameonesha wapi wasanii wa muziki huo wanatakiwa kwenda.Ndio maana kuna sehemu anawaambia sasa ni wakati wa kusema mapanga No.

Ukweli bado muziki wa singeli unasafari ndefu lakini walioanza ni vema wakakaza buti ili kuufikisha mahali ambapo kila mmoja wetu ataelewa nini maana ya singeli.

Najua kuna wengine wanasubiri kuona siku ambayo wasanii wa singeli wakishirikiana na wasanii wengine huko duniani kuimba muziki huo.Juhudi na maarifa kwa wasanii wa muziki huo ndio njia sahihi ya kuwafikisha ambako wengi wanatarajia. Usiwe ni muziki wa vijana tu.

Usiwe muziki kwa ajili ya wahuni peke yao au muziki wa watu waliokata tamaa ya maisha.Singeli ifike mahali iwe muziki unaopendwa na kila mtu na hili litawezekana.

Najua wengi wanaoimba muziki huo bado hawajaanza kufikisha ujumbe wanaokusudia na ndio maana sehemu kubwa umetawaliwa na kelele.Itoshe tu kusema wameanza vizuri kubwa ni kuendeleza Singeli.

Nafahami ili jambo lifanikiwe ipo haja ya kuwaambia ukweli. Hivyo Zeze kwa kutumia mamlaka yake katika uwanja wa sanaa na burudani linaona haja ya kuwakumbusha akina Man Fongo ,Msaga Sumu na wenzao wengine kuwa singeli inatakiwa kukubalika na kila mtu na si wao kwa wao.

Sawa hata kama haina ushemeji bado iko haja ya kuangalia namna sahihi ya kuufikisha muziki huo katika kiwango ambacho kitakubalika na walio wengi.Singeli imekuja na kasi kama vile ile ya mtandao ya 4G lakini wanajua wanakokwenda?

Kwa maoni -0713833822
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo