Wafuasi wa Gwajima watinga na sare kortini


WAFUASI wa Askofu wa Kani­sa la Ufufuo na Uzima, Jose­phat Gwajima juzi walitinga mahakamani kumsindiza Askofu wao wakiwa wamevaa sare ya suti nyeusi, tai nyeusi na nyekundu.

Mwonekano wao ulis­hangaza watu waliokuwa kwenye Mahakama hiyo ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.

Waumini hao waliofurika mahakamani hapo muda wote walikuwa vikundi vi­kundi wakisubiri kusikilizwa kwa kesi ya kutoa lugha ya matusi dhidi ya Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, inayomkabili Gwajima.

Kesi hiyo ilikuwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Mfawi­dhi, Cyprian Mkeha kwa ajili ya kutajwa na kuangalia rufaa iliyokatwa Mahakama Kuu na Jamhuri, kuhoji kwa nini CD inayomwonesha Askofu Gwajima akitoa maneno hayo kama kielelezo katika kesi hiyo, ilikataliwa.

Hakimu Mkeha alisema kesi hiyo imechukua miezi minne bila chochote kuendelea kuto­kana na rufaa hiyo kukatwa, kwa hiyo kama upande wa Jamhuri una nia ya kuondoa rufaa hiyo, iiondoe.

Kutokana na hoja hiyo, Wak­ili wa Serikali, Jackline Nyan­tori alidai kuwa wana nia ya kuondoa rufaa hiyo ili kesi iendelee ilipoishia.

Baada ya hapo, Hakimu Mkeha aliiahirisha hadi Sep­temba 29 itakapoletwa kuta­jwa na kuangalia upande wa Jamhuri ulikoishia na rufaa yao, ambapo pia Hakimu al­imtaka shahidi aliyefika ma­hakamani kutoa ushahidi, awepo siku hiyo.

Awali Mahakama ilitupilia mbali maombi ya kupokea kielelezo hicho cha Jamhuri kwa kushindwa kutimiza kig­ezo cha kisheria cha vielelezo vya eletroniki mahakamani.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo