Mwingereza aolewa Lindi, anywa pombe za kienyeji



MKAZI wa Lindi, Dennis Marcus na mkewe raia wa Uingereza, Antonia Martin, wamefunga ndoa kwa sherehe ya aina yake wakipanda bajaji na kunywa pombe ya kie­nyeji pamoja na wageni waalikwa.

Akizungumza na gazeti hili kwa simu jana, Marcus alisema harusi hiyo ilifanyika Namanga, Lindi na waliamua iwe hivyo, ili kuonesha tofauti kati ya mila na utama­duni wa kiafrika na wa kizungu.

Alisema harusi hiyo ilifuata muda wa harusi za kawaida, lakini waalikwa wali­kula wali kwa maharage, pilau na kunywa pombe za kienyeji ili kuonesha utofauti huo.

“Nilitaka harusi iwe tofauti sana kwa kuwa kama ni gari lilikuwapo, hivyo hai­kuwa na haja ya sisi kulitumia, nikaamua kutumia bajaji kwa sababu si kitu kina­chotumika katika harusi mara kwa mara,” alisema.

Mavazi

Kwa mujibu wa Marcus, gauni la harusi la mkewe lilishonwa nchini kwa ubunifu wake ingawa viatu, suti na ua la bibi harusi vilitoka Uingereza.

Akielezea historia yao, Marcus alisema walikutana na mkewe huyo mwaka 2008 Uingereza akiwa kwenye michezo ya sarakasi.

“Huwa nakwenda mara kwa mara Uin­gereza kwa masuala yangu na sarakasi na huko nilikutana naye,” alisema na kuongeza kuwa mkewe alisindikizwa na binamu yake na mtoto wake aliyezaa kabla ya wao kukutana.

“Mimi ndiye nilianza kumpenda am­bapo mwaka 2008 nilikuwa nacheza ‘pool table’ ndipo akaja na rafiki yake nami ni­kamwambia jinsi ninavyojisikia,” alisema.

Alisema mwaka 2013 kulikuwa na mashindano ya sarakasi Uingereza am­bapo mkewe alikuwa meneja na baadaye mwaka 2014 walikutana tena Dubai wa­kaendeleza mapenzi yao na Januari mwaka jana mkewe huyo alikuja nchini.

“Nahisi huyu ni mwanamke sahihi kwangu, pia kutokana na umri wangu kwenda, hivyo nahitaji mke wa kuishi naye kama vitabu vya dini vinavyosema,” alisema.

Marcus alisema aliona huyo mwanamke ndiye chaguo sahihi kwake na kuishi pamoja na kuzaa watoto na kujenga mai­sha ya baadaye.

Marcus alisema Julai 23 walifunga ndoa hiyo kwenye Kanisa Katoliki, Lindi na ali­yewafungisha ndoa hiyo ni Padri Alkuine Innocent.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo