Mkono wa Maalim wamtesa Magufuli



RAIS John Magufuli ameone­kana kuteswa na kusikitishwa na kitendo cha Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, kumnyima mkono Rais wa Zan­zibar, Dk Ali Mohamed Shein al­ipomsalimia wakati wa maziko ya Rais wa Awamu ya Pili Zanzi­bar, Aboud Jumbe Mwinyi.

Masikitiko hayo aliyatoa jana wakati akihutubia kwenye mku­tano wa hadhara wa kushukuru wananchi wa Zanzibar kwa kum­chagua kuwa Rais wa Tanzania, katika viwanja vya Demokrasia Unguja, ambako alitumia muda mrefu kufafanua kuhusu mkono huo kwa kauli tofauti tofauti.

Alisema Dk Shein kwa upendo na moyo wake wa huruma, alia­mua kumpa mkono mtu fulani (Maalim Seif), lakini cha kush­angaza alikataa kupokea mkono na kibaya zaidi ilikuwa msibani.

“Juzi wote tumeshuhudia msibani na Watanzania wameo­na kwenye picha, Dk Shein kwa unyenyekevu alimsalimu mtu fulani, lakini akakataa. Mkono huo huo ambao ameukataa, ndio Rais Shein anautumia kusaini fedha za safari na matibabu.

“Kweli una moyo wa upendo, natamani ningekuwa na hata robo maana mimi nisingeweza kutumia mkono wangu kum­sainia mtu akatibiwe, wakati mkono huo huo aliukataa,” alisema Dk.Magufuli.

Dk Magufuli alisema pamoja na mambo mengine, bado an­ampongeza Rais Shein kwa upole, ukarimu na uungwana kwani licha ya kupata asilimia 92 ya kura zote, ameingiza wap­inzani kwenye serikali yake.

‘Hataki’ wapinzani
Alisema yeye hawezi kumuin­giza mpinzani kwenye Serikali yake kama alivyofanya Dk Shein na kufafanua kuwa ndani ya Serikali yake, hatakuwa tayari kumuingiza mpinzani afanye naye kazi.

“Rais Shein muombe Mungu akupe hata robo ya mawazo yan­gu. Natamani niwe na moyo wa aina yako lakini siwezi maana kama mimi ningekuwa nime­kataliwa mkono, tena msibani, nisingesaini hata kidogo fedha kwa ajili ya huyo mtu.

“Jana (juzi) nikiwa Pemba ni­likuomba uongeze ukali hata kidogo. Kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 uchaguzi umekwisha na hautar­udiwa tena ila uchaguzi mwing­ine ni mwaka 2020. Kwa sasa ni muda wa kufanya kazi tu,” ali­sisitiza Dk. Magufuli.

Alisema anafahamu kuwa Zan­zibar kuna tatizo la maji lakini tayari kuna fedha Sh bilioni 200 zimetengwa kwa ajili hiyo, am­bapo alirudia kuwa hata kama kuna watu wanamnyima miko­no, aendelee na jukumu la ku­hakikisha wananchi wanapata maji.

Magufuli alisema lazima watu watambue walikotoka, walipo na wanakokwenda kwa kuwa sasa Zanzibar ni tofauti na ile ya zamani.

Alikumbusha alipokuwa Wa­ziri wa Ujenzi, kwamba alisi­mamia upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Zanzibar na anakum­buka hiyo ilikuwa ni kwenye utawala wa Awamu ya Tatu chini ya mzee Benjamin Mkapa.

Alielezea kushangaa kuona mtu anatoka Zanzibar na kwen­da kuwaambia wageni wasije Zanzibar, lakini cha kufura­hisha wamempuuza na wageni wameendelea kuja maana kuna usemi unaosema kuwa mgeni njoo mwenyeji apone.

*Kufuga ndevu

Magufuli alisema katika mai­sha yake hakuwahi kufikiria kuwa Rais, maana alitambua kuwa vyeo vinaletwa na Mungu na kama Mungu amesema hapa­na ni hapana tu, hata kama un­afuga ndevu namna gani kama Mungu amekataa huwezi kuwa Rais.

“Rais Shein ana moyo wa up­endo kwa watu wote lazima aachwe afanye kazi yake maana Wazanzibari wameamua ndio awe Rais,” alisema na kuongeza kuwa wakati Rais Shein anafan­ya mambo yote kwa ajili ya Zan­zibar, anatokea mtu anamnyima mkono mbele ya waombolezaji waliopo msibani.

Alifafanua kuwa hakuna kita­bu chochote au dini yoyote du­niani kinachofundisha chuki badala yake pale watu wan­apokoseana, basi wasameheane.

“Lakini hata kwenye msiba uu­uwiii,” alisisitiza Rais Magufuli na kuongeza anatamani kuona nchi inakuwa ya viwanda ili watu wengi wapate ajira kwani hakuna mtu anayekula chama cha siasa.

Aliomba wananchi wa Zan­zibar wadumishe umoja na mshikamano na kuweka chuki pembeni, kwani ni jambo baya kuona kuna watu wanafanya kazi ya kufarakanisha watu.

“Mnamkuta mtu na dada yake mmoja CUF na mwingine CCM wewe unamfarakanisha. Una­kuta mtu na mkewe mmoja CUF na mwingine CCM unawafara­kanisha mpaka wanashindwa kulala chumba kimoja, huu ni sawa na ushetani,” alisema.

*Fyoko fyoko

Wakati huohuo Rais Magufuli ameonya kuwa katika utawala wake, amani ataipa kipaumbele na yeyote atakayeleta fyoko­fyoko itamrudia mwenyewe.

Alisema msimamo wake hau­tabadilika na anayetaka kuvu­ruga amani atamshughulikia kwani hatamuachia iwe mchana au usiku, iwe asubuhi au jioni na hata akiwa kitandani, atakaye­jaribu kuleta chokochoko lazima atamshughulikia.

Magufuli alisema amekwenda Zanzibar kwa dhamira ya ku­waeleza wazi kuwa katika urais wake, amani itakuwa kitu cha kwanza ndio maana aliwahi kusema Dar es Salaam atakayele­ta fyoko fyoko, atakiona cha mtema kuni.

Alisisitiza kuwa msimamo wake wa pili ni kudumisha Muungano uliopo kati ya Tan­zania Bara na Zanzibar kwa ku­ulinda kwa nguvu zake zote.

Kipaumbele chake cha tatu, alisema ni kuleta maendeleo ya wananchi wote bila kujali vy­ama vyao. “Iwe CCM, iwe CUF, iwe Chadema na hata wasio na vyama wote nitahakikisha nale­ta maendeleo yao,” alisema.

*Dk Shein

Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha Rais Magu­fuli, Dk Shein alisema vyama vya upinzani vitaiona Serikali ya Zanzibar kama ilivyo, kwa kuwa kwa kutumia utaratibu wa kidemokrasia CCM hawang’ooki kwani kila uchaguzi watashinda na kuwagaragaza.

“Baada ya uchaguzi zikatoka kauli kwamba utarudiwa tena, masikini roho zao, nami huwa nawauliza utarudiwa kwa Katiba gani, na kwa sheria gani? Maana chini ya Tume ya Uchaguzi ya Mwenyekiti Salimu Jecha, uch­aguzi umemalizika.

“Sheria na Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 ndio iliyotoa mamlaka kwa Tume ya Uch­aguzi kuendesha uchaguzi wa rais, wabunge, madiwani na wawakilishi. Ni katiba ya Zan­zibar hakuna katiba nyingine duniani inayoweza kuitisha uchaguzi tena, hizi ni hadithi ziacheni mitaani, ukweli tuta­kutana mwaka 2020 wakati wa Uchaguzi Mkuu,” alisema.

Alisema hakutakuwa na Seri­kali ya mpito Zanzibar na wa­naosema hivyo wanajidanganya kwani hakuna sababu ya kuwa na serikali ya aina hiyo, kwa sababu Serikali imeshakuwa ma­darakani.

*Mafuta na gesi

Kuhusu mafuta na gesi Zanzi­bar, alisema limepatiwa ufum­buzi wa kudumu kwa kush­irikiana na Rais mstaafu Jakaya Kikwete, ambapo walitunga She­ria ya Mafuta na Gesi na kwa sheria hiyo, Zanzibar ilipewa mamlaka ya kutunga sheria yake ya mafuta na gesi na imeshapele­kwa kwenye Baraza la Wawakili­shi na kikao kijacho cha Septem­ba 26, itasomwa tena.

“Baraza wakiipitisha watai­leta kwangu, nitasaini na kuwa sheria na kuanza kutumika, baada ya hapo tutaanza kuita wawekezaji na Zanzibar itaanza kupiga hatua kwa kuwa tuna mambo mazuri ya mafuta na gesi,” alisema.

Alisema atashirikiana na Rais Magufuli kutekeleza sheria hiyo, pamoja na kuiwezesha Zanzibar kukuwa kiviwanda hasa vya sa­maki.

Aliongeza kuwa Zanzibar imeendelea kukusanya kodi ipasavyo, kwani hivi sasa ma­pato yameongezeka kwa kiasi kikubwa. Alitoa mfano wa 2011 walipokuwa wakikusanya Sh bil­ioni 13 kwa mwezi, wakati sasa wanakusanya Sh bilioni 52.

“Pesa hazitutoshi lakini tu­nazo, tumewalipa wastaafu takribani Sh bilioni 16, tunatoa mishahara kwa wakati na utalii umetuingizia fedha za kigeni kwa zaidi ya asilimia 80,” alise­ma.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo