Edward Lowassa |
ALIYEKUWA Naibu Katibu wa
Bunge, John Joel, ametaja mambo matatu ambayo hatayasahau katika utumishi wake
bungeni.
Akizungumza katika
mahojiano maalumu na Jambo Leo Dodoma mwishoni mwa wiki iliyopita, Joel alitaja
mambo hayo kuwa ni sakata la Richmond, Escrow na G55, akieleza kwamba
yaliibuliwa kwa sababu za kutafuta madaraka.
Alisema katika maisha yake
ya utumishi hatasahau sakata la Richmond lililomfanya aliyekuwa Waziri Mkuu,
Edward Lowasa ajiuzulu. Hata hivyo, alisema kama Bunge la kipindi hicho mwaka
2008 lingejikita katika kufanya uchunguzi wa kina, huenda yaliyotokea,
yasingetokea.
"Hapakuwa na
uchunguzi wa kina juu ya masuala hayo," alisema Joel ambaye sasa amestaafu
baada ya kuhudumu katika ofisi ya Bunge kwa miaka 24.
Katibu huyo wa Bunge wa
zamani, ambaye alianza kazi enzi za Bunge la chama kimoja, alisema ataendelea
kulikumbuka kundi la G55 kwa hatua yake ya kutaka kudai uwepo wa Tanganyika,
akisema bila marehemu Mwalimu Julius Nyerere kuingilia kati, sakata ilo
lingeing’oa Serikali na kuvunja Muungano.
Joel alisema katika
utumishi wake bungeni tukio la Richmond alilifananisha na sakata la Escrow na
kueleza kwamba ilikuwa ni vita ya madaraka.
Alisema kwa kuanzia na
sakata la Richmond ambalo lilimfanya Lowasa kuwajibika kwa kijihuzulu mwaka
2008, sakata ilo halikufanyiwa uchunguzi wa kina na badala yake lilimalizwa kwa
woga.
“Kwa mfano sakata la
Richmond, ilibidi aliyekuwa Waziri Mkuu awajibike, lakini ukilichunguza kwa
undani kabisa, utaona halikuwa limefanyiwa utafiti wa kutosha, lilitufikisha
tulipofika sababu ya woga," alisema Joel.
Alisema kupitia sakata
hilo, pande mbili zilizokuwa bungeni, zililibeba kwa sura mbili tofauti huku
akifafanua kuwa CCM walilibeba kwa woga na kuona kuwa wasingelipatia ufumbuzi
lingeweza kuiangusha Serikali, huku wapinzani wakilichukulia kwa sura ya hoja
ya kuingilia madaraka.
Aliongeza kuwa sakata hilo
halikuwa limefanyiwa uchunguzi wa kina kwa kuangalia chimbuko la tatizo, na
badala yake wahusika walijikita zaidi kwa kutazama mtu na kwamba ungekuwapo ufuatiliaji
mzuri yasingetokea yaliyotokea ambayo alidai yalileta uadui pia.
"CCM waliona pesa
nyingi zimetumika, kwa hiyo wakaona wasipolibeba wao Serikali ingeweza
kuanguka, lakini kwa Upinzani nao walitaka kulibeba kwa sura ya kuona kama
wangeweza kutumia hoja hiyo kuingia madarakani.
"Lile suala lingekuwa
limefanyia uchambuzi wa kina kwa kuangalia tatizo lilipo, halafu lifanyiwe kazi
tatizo badala ya kujihusisha na watu, pengine tusingefika tulikofika na pengine
tusingefikia hali ya kuwa na uadui ambao ulijitokeza.
"Kulikuwa na haja ya
kufanywa uchunguzi wa kina, wangekwenda kushughulika na hayo, badala ya watu na
madaraka," alisema Joel. Sakata la Richmond lilihusu ufisadi uliotokana na
uagizaji wa mitambo ya kufua umeme ili kukabiliana na tatizo la umeme
lililoikumba nchi wakati huo.
Akioanisha sakata hilo na
la Escrow lililoibuliwa bungeni siku za karibuni, Joel alisema matukio hayo
yanafanana na yakitazamwa kwa kina bado yanahusu madaraka na si zaidi ya hapo.
Saka la Escrow lilitokana
na ukaguzi maalumu wa akaunti ya Tegeta Escrow ulioombwa na Katibu wa Bunge na
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini ufanywe na Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti
Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Ukaguzi huo ulilenga
kufanya uchunguzi wa kina aili kutoa taarifa kamili yenye kuonesha hali halisi
kuhusu miamala kwenye akaunti maalumu ya Tegeta Escrow kisha kutoa taarifa.
"Sakata la Richmond
ni sawa na Escrow, nakumbuka tulifanya kazi tangu saa tatu asubuhi mpaka saa
nane usiku, lakini ukiangalia kwa undani ni madarakaÖni madaraka tu hakuna kitu
kingine," alisema.
Aliongeza kuwa suala la
madaraka liligusa CCM na Upinzani, na ndiyo maana sakata hilo liliibuliwa
kipindi cha mwelekeo wa Uchaguzi. Escrow iliingia wakati wa kipindi cha
kuelekea uchaguzi, ilikuwa ni kutafuta nani anaingia madarakani kila upande
ukitaka kutazama nani anabaki nani anangÃoka," alisema.
"Escrow ilikuja kama njia
ya kutafuta madaraka, Upinzani waliitumia baada ya kushindwa kwenye Richmond,
na ukiangalia uanzishwaji wa Escrow upo kisheria, lakini ikaingizwa ndani ya
Bunge kama ajenda ya kisiasa, lengo kubwa Serikali ianguke, vivyo hivyo kwa CCM
ilikuwa Fulani asichukue madaraka, Fulani aachwe," alisema Joel.
Kundi
la G55 Kuhusu sakata la kutaka kuvunjwa kwa Muungano kwa kudaiwa kwa Tanganyika liloibuliwa na kundi la wabunge 55 mwaka 1993 likiitwa G55, Joel alisema hatasahau sakata hilo, kwa kuwa lilitikisa nchi na Serikali.
Alisema kundi ilo la
wabunge lilokuwa likiongozwa na aliyekuwa Mbunge wa Lupa Njelu Kasaka (CCM),
lilitikisa kwa kuwa lilikuja bungeni na hoja nzito iliyogusa mustakabali wa
nchi.
Kundi hilo lilitaka
Muungano upitiwe upya na ikiwezekana uboreshe na kurejeshwa kwa Serikali ya
Tanganyika. Joel alisema hatalisahau na kufafanua kuwa kwa mara ya kwanza
alimshuhudia Mwalimu Nyerere akilazimika kuingia bungeni kutafuta suluhu.
"Kundi lile la G55
lilitikisa nchi, liliyumbisha nchi sababu ilikuwa inahusu Muungano, lakini
ilikuwa ni kwa ajili ya kujenga misingi iliyo imara. "Kama si Nyerere,
nadhani Muungano usingekuwapo tena, sababu tulifika pabaya sana, suala hilo
lilipatiwa suluhu baada ya kukubali kutokubaliana na Mwalimu Nyerere alilazimika
kuingilia kati," alisema Joel.
Mbali na Kasaka wengine
waliounda kundi hilo ni Lumuli Kasupa (Kyela), William Mpiluka (Mufindi), Mateo
Qaresi (Babati), Jared Gachocha (Ngara), Tito ole Kipuyo (Arusha), Philipo
Marmo (Mbulu), Arcado Ntagazwa (Muhambwe) na Patric Qorro (Karatu).
Wengine ni Japhet
Sichona(Mbozi), Jenerali Ulimwengu (Taifa), Abel Mwanga (Musoma Mjini), Profesa
Aaron Massawe (Moshi Vijijini), Shashu Lugeye (Solwa), Sebastian Kinyondo (Bukoba
Vijijini), Phares Kabuye (Biharamulo Magharibi) na Mbwete Hombee (Rungwe). Pia
Kisyeri Chambiri (Tarime), John Byeitima(Karagwe), Abdalah Nakuwa (Lindi),
Ndembwela Ngunangwa(Njombe Kusini), Mathias Kihaule (Ludewa), Mussa Nkhangaa
(Iramba), Edward Ayira (Rorya), Adam Karumbeta (Mbeya) na Halimeshi Mayonga
(Kigoma Vijijini).
Wabunge wengine ni Dk John
Katunzi (Geita), Ismail Iwvata (Manyoni Magharibi), Tobi Mweri (Tanga), Aidan
Livigha (Morogoro), Tabitha Siwale(Taifa), Obel Mwamfupe (Mbeya), Othman
Mpakani, Evarist Mwanansao (Nkasi) na Paschal Degera (Kondoa Kaskazini).
Hali kadhalika Erasto
Losioki (Ngorongoro), Nasoro Malocho (Mtwara), Charles Kagonji (Mlalo), Venance
Ngula (Taifa), Benedicto Lusurutia (Kiteto), Dk Deogratius Mwita (Serengeti
Pius Nko (Arumeru), J. Mwanga na Chadiel Mgonja (Same), Pia walikuwamo Guntram Itatiro
(Ifakara), Paschal Mabiti (Mwanza), Edith Munuo (Taifa), Raphael Shempemba
(Lushoto), John Mhina (Muheza), George Nhigula (Kwimba), Kapteni Thadeus
Kasapira (Ulanga Magharibi), Charles Kinuno (NyangÃhwale), Christian Fundisha
(Tabora Kusini), Samwel Rwangisa (Bukoba Mjini) na Maria Kamm (Taifa).
0 comments:
Post a Comment