WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, amesema Serikali ya Awamu ya Tano imekusudia kufuta umaskini kwa Watanzania.
Pia aliwahimiza wananchi
waliopitiwa na mpango wa umeme vijijini kuunganishwa na nishati hiyo ili
kuondokana na matumizi ya vibatari.
Muhongo alisema juzi kuwa
wananchi wanatakiwa kuchangamkia fursa ya Mradi wa Rea hasa ikizingatiwa kwamba
gharama ya kuunganishiwa umeme ni Sh. 27,000. Alisema mwisho wa malipo ni
Oktoba 30, mwaka huu.
Katika mazungumzo yake na
wananchi wa Kata ya Dindira, Tarafa ya Bungu, Prof. Muhongo alielezea kushangazwa
kwake na mwamko mdogo wa wananchi kuunganishiwa umeme licha ya kutozwa gharama
ndogo.
Alisema serikali
imejipanga kuwakwamua wananchi wake ambapo wakitumia fursa ya nishati ya umeme
vijijini kujianzishia miradi ya uzalishaji mali wataimarisha uchumi wao.
"Ndugu zangu hali ikiendelea hivi haitawezekana Mradi wa Rea awamu ya tatu
kuja tena wataangalia kwenye ëspeedà kubwa, hivi sasa tu hamjaweza kumaliza
nafasi zenu waliojiunga ni wateja 470 wakati matarajio ni zaidi ya wananchi
1,200," alisema.
Muhongo alimtaka Meneja wa
Tanesco Wilaya ya Korogwe, Dominic Mwikanu kufika Dindira kuwaelimisha wananchi
ili kuunganishiwa umeme huo. Alisema serikali imejipanga kufikisha nishati ya
umeme kwenye vijiji vyote ambapo Rea awamu ya tatu mbali na kufika vijiji
vitakavyokuwa vimeainishwa kipaumbele kitatolewa kwa nyumba za ibada, shule,
zahanati, nyumba za biashara na vyama vya siasa.
Katika ziara hiyo,
alitumia fursa hiyo kukanusha uvumi uliozagaa kwa wananchi kuwa Rea ni mradi
ambao umeletwa na Rais wa Marekani, Barack Obama.
Alisema mradi huo
unatokana na kodi za wananchi na unaendeshwa na serikali yao. Muhongo alitoa
ufafanuzi huo baada ya Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stephen Ngonyani kumweleza
kwamba baadhi ya watu wamekuwa wakimkebehi kuwa nishati hiyo ya umeme
haikufikishwa maeneo yao kwa nguvu za serikali.
"Huu si umeme wa
Obama, ni fedha za walipa kodi, kila uchao mbunge wenu amekuwa akijitahidi
kunikumbusha kuhusu umeme, safari ya umeme nimeanza naye na ningependa tumalize
wote, msimuangushe," alisema Prof. Muhongo.
0 comments:
Post a Comment