NAIBU Spika wa Bunge Dk. Tulia Ackson
amesema hakuna mbunge mwenye hadhi ya juu kuliko mwingine katika Bunge na
kwamba Katiba inatambua na kueleza kuwa wabunge wote wapo sawa.
Aidha alisema katika utendaji wake hana
upendeleo kwa mbunge yoyote bali hutekeleza wajibu wake kwa kufuata sharia na
kanuni zinazoliongoza Bunge.
Akizungumza kwenye mahojiano na kituo
cha televisheni cha ITV, Dk. Tulia alisema makundi yote ya wabunge
yakishaapishwa huwa ni wabunge wanaofanana kwa hadhi ya kufanya kazi wanapokuwa
bungeni.
“Katiba ilivyoyaweka makundi matano ya
wabunge kuanzia wanaoteuliwa na Rais, wanaochaguliwa na wananchi, wabunge wa
viti maalum na wanaotoka Baraza la Wawakilishi Zanzibar na Mwanasheria Mkuu wa
Serikali, wote wamewekwa kwa sababu maalumu kwa sababu hiyo wabunge wote ni sawa,"
alisema Dk. Tulia
Aidha Naibu Spika ameitaka jamii
kubadilika kutoka katika dhana kwamba mwanamke ambaye anashika nafasi ya juu
katika uongozi kwamba amebebwa na waamini kuwa vigezo na masharti
vinazingatiwa.
“Wanawake wengi ambao wamepewa nafasi ya
uongozi kwa kuchaguliwa au kuteuliwa ni mara chache sana hufanya vibaya na hata
akifanya vibaya jamii humhukumu kwa kuwa ni mwanamke wakati kuna wanaume katika
nafasi kama hiyo ambao pia unakuta wamefanya vibaya hivyo kuna changamoto hiyo
katika jamii," alisema.
Katika hatua nyingine alisema anaongoza
Bunge bila upendeleo wowote ila anafuata sheria na kanuni za kuongoza Bunge.
Pia alizungumzia tatizo la upnde wa
wabunge wa upindani kutoka nje bunge likiwa linaendelea ambapo alisema
"katika hali ya kawaida ukiwa kiongozi lazima ujifunze kuishi na watu wa
kila aina, wakiwa pale ndani wakiwa kundi wakitoka ndo mtu unaona sijui
wamefanyaje, lakini mimi ndiye ninayeshughulika na mambo yao ya kila siku
ofisini pale.”
0 comments:
Post a Comment