Sharifa
Marira
MWENYEKITI
wa Chadema, Freeman Mbowe, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama hicho, Edward Lowassa
na viongozi wengine waandamizi wameitwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar
es Salaam kwenda kuripoti kesho.
Hatua
hiyo inatokana na viongozi hao kukamatwa juzi, baada ya kufanya mkutano maalumu
wa ndani wa Kamati Kuu, na walipelekwa Kituo Kikuu cha Polisi cha Kanda hiyo na
kuhojiwa kabla ya kuachiwa.
Mbali
na Mbowe na Lowassa, viongozi wengine wa Chadema waliokamatwa na kutakiwa
kwenda Polisi kesho ni Katibu Mkuu, Vincent Mashinji, Naibu wake, John Mnyika
na Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho, Said Issa Mohammed.
“Wameitwa
Polisi waende Septemba mosi kuripoti baada ya jana kukamatwa na kuhojiwa wakituhumiwa
kukiuka maagizo ya Polisi,” alisema Msemaji wa Chadema, Tumaini Makene na
kufafanua:
“Lakini
wanaweza kwenda au wakaanzia kwenye maandamano kisha wakaenda Polisi kuripoti.”
Alisema
maandamano hayo yatakuwapo kama yalivyopangwa kwani maandalizi yake
yamekamilika.
Habari
zaidi zilieleza, kwamba jana mchana viongozi hao walikuwa wakifanya kikao Makao
Makuu ya chama hicho Kinondoni Dar es Salaam, ambapo pia walikutana na wabunge
wote wa chama hicho kwa makundi tofauti.
Kwa
mujibu wa mtoa habari ndani ya Chadema makao makuu katika kikao hicho pamoja na
suala la utekelezaji wa Ukuta kesho.
Mmoja
wa wabunge wa Chadema aliliambia gazeti hili, kwamba walikuwa wakiwekana sawa
kuhusu maandamano yao.
Alibainisha
kwamba katika mkutano huo ambao Mbowe hakuwapo pia walijadili maombi ya
viongozi wa dini kuwataka kusitisha maandamano hayo Septemba mosi.
“Viongozi
wa dini wamekuwa wakituomba tusitishe maandamano ya Ukuta Septemba mosi,
tusubiri hadi baada ya mkutano wa vyama vya siasa Septemba tatu,” alisema Mbunge
huyo wa Kanda ya Ziwa.
Aliongeza:
Katika mkutano huo, Lowassa na viongozi wengine walijadili hayo na ikikubalika
kwa heshima ya viongozi wa dini maandamano ya Ukuta yafanyike baada ya Septemba
tatu.”
Hata
hivyo, JAMBO LEO ilishuhudia wabunge wengi wa chama hicho wakitoka katika
mkutano huo kimya kimya bila kutaka kuzungumza na kabla muda uliopangwa kwisha,
huku taarifa zikieleza kwamba mkutano huo uliahirishwa baada ya kuwepo taarifa
za kutaka kuvamiwa na Polisi.
“Tumeambiwa
tusambaratike, tutajulishwa wapi tutakutana tena, kama hapa au wapi,” alidokeza
mmoja wa wabunge hao.
Baada
ya mkutano huo kuahirishwa, Lowassa alitoka eneo hilo huku taarifa zikieleza
alikuwa akielekea kwenye moja ya hoteli jijini humo kuungana na Mbowe ambapo
walikuwa na mazungumzo na baadhi ya viongozi wa dini.
0 comments:
Post a Comment