Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Dk. Modestus Kipilimba |
Na Lilian Lundo wa MAELEZO
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
(NIDA) imeeleza kuwa ifikapo Desemba 31 Watanzania milioni 23 watakuwa na namba
za utambulisho wa vitambulisho vya uraia. Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
wa Mamlaka hiyo, Rose Mdami alisema jana kuwa hatua hiyo ni utekelezaji wa
agizo Rais John Magufuli kwa NIDA kuweka saini ya mwombaji na mtoa
vitambulisho.
"Tulianza kutekeleza agizo la Rais
tangu Juni, inamaanisha vitambulisho vyote tulivyochapisha kuanzia Juni vina
sainihizo mbili na tarehe ya kuzaliwa mwombaji," alifafanua Mdami.
Alieleza kuwa ugawaji wa vitambulisho
hivyo unasubiri uzinduzi wa Rais Magufuli atakayekabidhiwa kitambulisho namba
moja na baadaye vitagawiwa kwa wengine. Alisema ili mwananchi apate
kitambulisho cha uraia, lazima afike ofisi za NIDA akiwa na vielelezo
vinavyoonesha mwaka wa kuzaliwa uthibitisho wa uraia hii ni kutokana na NEC
kutokuwa na viambatanisho hivyo.
Alibainisha kuwa mwananchi mwenye namba
ya utambulisho anaweza kupata huduma zote kutokana na namba hiyo kutobadilika
na kutumika hata baada ya kitambulisho kuchapishwa.
Alisema mpaka sasa Watanzania milioni
2.7 wamepewa vitambulisho††hivyo na milioni 6.5 wamesajiliwa kwa ajili ya
kupewa. Aidha, vitambulisho vya zamani vitaendelea kutumika mpaka
utakapotangazwa utaratibu wa kuvibadilisha na kupata vipya.
Alitoa ufafanuzi juu ya malalamiko ya
baadhi ya watu kwamba kuna mlolongo mrefu wa kupata vitambulisho hivyo kwa kuwa
NIDA haina namna ya kufupisha mlolongo huo, kwani kufanya hivyo ni sawa na kuuza
uraia wa Tanzania.
0 comments:
Post a Comment