William Shao
WATAFITI wamegundua kuwa ijapokuwa kuna njia na vifaa vingi vya mawasiliano kuliko wakati mwingine wowote katika historia, hakuna kipindi ambacho wanadamu ni wapweke kama ilivyo leo.
WATAFITI wamegundua kuwa ijapokuwa kuna njia na vifaa vingi vya mawasiliano kuliko wakati mwingine wowote katika historia, hakuna kipindi ambacho wanadamu ni wapweke kama ilivyo leo.
Simu za mkononi, ujumbe mfupi (SMS), Whatsapp, Instagram,
baruapepe, Facebook, Telegram, vituo vya mawasiliano na vituo vya
maongezi—hakujawahi kuwa na kipindi chochote katika historia ya mwanadamu
ambapo kuna njia nyingi za kuwasiliana kama ilivyo sasa.
Pamoja na njia zote hizo, watafiti wanadai kuwa katika dunia hii yenye
njia nyingi za mawasiliano, watu wengi, vijana kwa wazee, ni wapweke mno.
Watafiti wawili—John T. Cacioppo na William Patrick—katika
kitabu chao, ‘Loneliness— Human Nature and the Need for Social Connection’,
wamezungumza kwa undani kuhusu upweke huo.
Wamezungumzia uchunguzi mmoja uliosema kwamba “kutumia sana
Intaneti badala ya kuzungumza na mtu moja kwa moja, kunaweza kufanya watu
wajitenge na jamii na pia kuongeza hali ya kuhuzunika.”
Hekaheka za maisha ya kisasa zinafanya iwe vigumu kwa watu
kuwasiliana kwa njia inayofaa. Kwa kawaida, unadai utafiti huo, huwezi kuona
uso unaotabasamu na upendo unapowasiliana na mtu kupitia simu au kwa kutuma
ujumbe kupitia kompyuta.
Mambo yaliyotajwa hapa juu hutokea pia katika familia. Katika
nyumba nyingi, watu wa familia huja na kuondoka bila kula pamoja au kuzungumza
pamoja. Vijana wana kompyuta na simu zao wenyewe nao hujitenga na watu wengine
wa familia. “Licha ya kwamba wana vifaa vingi vya mawasiliano, vijana wengi
hujihisi wakiwa na wapweke,” wanasema watafiti hao.
Siku hizi hata ndoa zinaweza kuhatarishwa kwa sababu ya wenzi
kujihisi wakiwa, wapweke. Wenzi wa ndoa wasipowasiliana, wanaweza kuwa katika
nyumba moja lakini kila mtu anaishi maisha yake. Kuhisi upweke huku ukiwa
unaishi na mwenzi wa ndoa ni upweke unaofadhaisha sana. Mbali na vitu vingine
vingi, kuwepo kwa vifaa vingi zaidi vya mawasiliano kunaweza kukatiza
mawasiliano kati ya mzazi na watoto na hivyo kufanya hisia za upweke
ziongezeke. Pia waseja wengi wanatamani kuwa na mwenzi, lakini mahitaji yao ya
kihisia hayatoshelezwi.
Upweke umekuwa tatizo kubwa katika jamii, tatizo ambalo linaweza
kusababisha uraibu wa pombe, kula kupita kiasi, kutumia dawa za kulevya,
kufanya ngono za ovyo, na hata kujiua.
Nchini Japani, Profesa Tetsuro Saito alisema: “Simu za mkononi na
vifaa vingine vinapunguza uwezo wetu wa kuwasiliana na wengine kwa hisia.”
“Watoto wanaeleza ni kitu gani muhimu sana kwao, baada ya maisha
yao, kinachofuata kwa umuhimu ni simu za mkononi,” akasema Masashi Yasukawa,
Mkuu wa Baraza la Taifa la Ushauri wa Mitandao nchini Japani, alipokaririwa
na gazeti ‘The Sydney Morning Herald’ la Australia,la Januari 12, 2008. Utafiti
mwingine nchini huo ulichapishwa na gazeti ‘The Sunday Telegraph’ uligundua
hivi: “Teknolojia . . . inawafanya watu wajitenge kihisia. Watu … hutumiana
ujumbe mfupi au barua-pepe badala ya kuzungumza moja kwa moja.”
Utafiti unaojulikana kama ‘Loneliness and Mobile Phones’
uliofanywa nchini Uturuki kwa kufanyiwa wanafunzi zaidi ya 500 wa Chuo Kikuu
cha Firat, uligundua kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya matumizi makubwa ya
simu za mkononi na kuhuzunika pamoja na kuwa na soni au haya.
Vinajana hawa kila mmoja akiwa na chombo chake
cha mawasiliano ambacho kinaelezwa katika utafiti kusababisha upweke na haya au
soni.
0 comments:
Post a Comment