Richard Mwaikenda, Mbarali
WAKAZI wengi wa Rujewa, wilayani
Mbarali, waliofika kuangalia eneo ambalo jua litapatwa na mwezi, wamekuwa
hawaelewi jinsi tukio hilo litakavyokuwa.
Baadhi ya wakazi hao waliohojiwa na
mwandishi wetu katika eneo hilo la Relini, kwamba waeleze ?kitakachokea
(kesho), leo walijibu kuwa hawaelewi.
Jumanne Mavunde (45), aliyekutwa
akiwa amejiinamia kwenye baiskeli yake, alisema kuwa hata yeye hajui
kitakachotukia ila alisikia alipofika pale kuwa eti jua litapatwa na kwamba
walioandaa ndiyo wanaojua.
Naye Halima Abbas (35) ambaye ana
elimu ya sekondari kidato cha nne, alisema kuwa anasikia tu kwamba kuna kupatwa
kwa jua lakini hajui ni kitu gani. Pia alisema hakumbuki kama somo hilo
alilisoma akiwa shuleni.
Mkazi wa Rujewa mwenye jamii ya
kimasai, Joshua Ole Kaulule, alijibu kuwa
anachojua ni kwamba(kesho) leo, jua na mwezi vitagongana na kusababisha
giza zaidi ya hapo haelewi.
Mwanamke mfanyabiashara wa mchele,
Heri Kiluswa, alisema kuwa yeye alikuwa anapita barabarani alishawishiwa kwenda
pale baada ya kuona watu wengi wamekusanyika, lakini haelewi ni kitu gani
kitanyika na alipouliza aliambiwa kuwa kuna tukio la kupatwa na jua, ila bado
haelewi ni jambo gani.
Mwanafunzi wa Darasa la saba katika
Shule ya Msingi Ihanga, Goodluck Mwanpasha (13), alisema kuwa hajui lolote na
hata shule hajawahi fundishwa na baada ya kuona watoto wenzie wanamcheka
alitimua mbio na kutokomea.
Lakini Mwananfunzi wa darasa la tano
katika Shule ya Msingi Ibala, Adamu Chengula alikiri somo hilo kufundishwa,
hivyo kujibu kiufasaha kwamba kupatwa kwa jua ale inapotokea Dunia, Mwezi na Jua kuwa kwenye mstari mmoja
na mwezi ukiwa katikati huzuia miale ya jua na kusababisha giza katika uso wa
dunia.
Mwandishi wetu alipata wasaa wa
kuzungumza na Pasvolo Mwinuka Mwalimu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT)
Idara ya Sayansi, ambaye alieleza
kitaalamu juu ya kupatwa kwa jua.
Alisema kuwa tukio hilo hutokea
dunia, mwezi na jua vinapokuwa kwenye mstari mmojo na mwezi kuwa kati hivyo
kuziba mwanga jua kuifikia dunia.
Alija aina tofauti za kupatwa kwa
jua kuwa ni. Mosi; Kuziba kabisa mwanga wa jua kunaitwa kupatwa kwa jua
kikamilifu (Total Solar Eclipse).
Pili;Kiasi kidogo cha mwanga wa jua
kuifikia dunia (Partial Solar Eclipse) na miale ya jua itakuwa imezibwa kwa
kiasi kikubwa kwa asilimia 97, kitendo ambacho hutengeneza muonekano wa mfano
wa pete na tukio hili ndiyo litakalotokea leo Rujewa. Kupatwa kwa jua kutaanza
saa 4 asubuhi hadi saa 8 mchana.
Alisema kitendo hicho duniani
kitatokea hapa nchini eneo la Relini Rujewa, mkoani Mbeya na kutaja maeneo mengine patapoonesha kwa kiasi tukio
hilo ni wilayani Wanging'ombe, Njombe, Karibu na Ziwa Tanganyika pamoja na
baadhi ya Nchi ya DRC Congo.
Naye Mjumbe wa Kamati ya Utalii ya
Wilaya hiyo, alisema kuwa maandalizi yanaenda vizuri na tayari wametoa elimu
kwa wananchi juu ya tukio hilo muhimu na la kihistoria katika wilaya hiyo na
njci kwa ujumla.
Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri
wa Maliasili na Utalii, Jumanne Maghembe ambapo pia atakuwepo Mkuu wa Mkoa wa
Mbeya, Amosi Makalla na viongozi wengine.
0 comments:
Post a Comment