WAKATI Chadema jana ikiamua kuahirisha kuanza mikutano na
maandamano yasiyo na ukomo, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama hicho, Edward Lowassa
amesema atamtafuta Rais John Magufuli wazungumze.
Hatua hiyo ilifikiwa jana na chama hicho cha Upinzani kwa
ilichokieleza ni kuheshimu mwito wa viongozi wa dini walioomba kupewa nafasi
ya wiki mbili ili wazungumze na uongozi wanachi.
Wakati uamuzi huio uklifikiwa nakutangazwa, Lowassa alielezea
kukutana kwake na Rais Magufuli siku ya maadhimishio ay Jubilei ya miaka 50 ya
ndoa ya Rais mstaafu Benjamin Mkapa.
Alioserma siku hiyo wawiklin hao hawakuzungumza mambo mauiubwa
zaidi ya kusdalimiana na kupeana mikonmo na kujuliana hali, hivyio kuwapo haja
ya kukuitanma nma kluzungumza kwa kina. Lowassa alisema jana kuwa baada ya kusalimiana walipotana Rais Magufuli alimwambia
kwamba atamtafuta.
“Nimeona mitandao imeandika mambo
mbalimbali lakini kusema ukweli hakuna jambo lolote ambalo tumezungumza na
Magufuli tofauti na salamu na kuniambia kuwa atanitafuta,” alisema.
Kuhusu kusalimiana naye alisema
hakuwa na nguvu yoyote ya kumkatalia au kutomsalimia hasa ukizingatia katika
tukio hilo kulikuwa na viongozi wa kiroho.
“Nadhani nyie ni wenzangu na
mnaamini katika imani hivyo sikuwa na nguvu ya kukataa mkono wa Rais mbele ya
viongozi wa dini sijui nyie,” alisema.
UKUTA
Wakati huo huo, Chadema kimeahirisha
maandamano na mikutano iliyopanga kuanzia leo nchi nzima kikieleza kutii
viongozi wa dini waliooomba wapewe wiki mbili ili kuonana na Rais John
Magufuli, kutatua mgogoro uliopo.
Kabla ya kuahirishwa maandamano
hayo, Julai 26 Chadema kupitia Kamati Kuu ilijitokeza mbele ya waandishi wa
habari na kutangaza operesheni hiyo ilijulikana kwa jina la Umoja wa Kupambana
na Udikteta Tanzania (Ukuta), ambao umeweza kuwa gumzo katika nchi nan je ya nchi.
Akizungumza katika mkutano na
waandishi wa habari Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Hai Freeman Mbowe
alisema viongozi wa dini wa madhehebu yote makubwa hapa nchini, taasisi za
kiraia, balozi na vyombo vya habari wamewaomba wasitishe.
Mbowe alisema viongozi hao ni Mkuu Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania
(KKKT), Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Mkuu wa Kanisa la
Anglikana Tanzania, Mkuu wa Kanisa la Afrika Inland Tanzania, Katibu Mkuu wa
Baraza Kikrustu Tanzania, Mkuu wa Kanisa la Kipentakosti Kirismatiki Tanzania,
Mufti Mkuu wa Tanzania na Mufti Mkuu wa Zanzibar.
Aidha, alisema viongozi wa taasisi
za kiraia kama Kituo cha Haki za Binadamu Tanzania (LHRC), Taasisi ya Mwalimu
Nyerere, Jukwaa la Katiba na Jukwaa la Wahariri na wengine wengi wamewaomba
watoa muda wa wiki mbili ili kutoa sintofahamu.
Alisema katika mazingira hayo ya
taasisi na viongozi wa dini wamelazimika kuahirisha hadi Oktoba mosi iwapo
hakutakuwa na muafaka.
Mbowe alisema mgogoro huo wa kisiasa
unatokana na uvunjifu wa Katiba unaofanywa na Rais John Magufuli na vyombo
vyake vya dola hivyo hawapo tayari kukubaliana nao.
Alisema haki zao za kisiasa
zimetajwa katika Katiba hivyo ni wazi kuwa hawapo tayari kuona haki hiyo
ikipotea na kwamba wapo tayari kuondoa tofauti zao kwa njia ya mazungumzo.
“Sisi Chadema hatuwezi kuwakaidi
viongozi wetu wa dini kwa sababu yoyote kwani ni aibu kwa sisi kufanya hivyo
hasa ukizingatia tumelelewa na imani hivyo basi tunaahirisha maandamano hadi
Oktoba mosi iwapo hakutakuwa na muafaka,” alisema.
Mbowe alisema wanaomba wadau na
makundi mbalimbali kushirikiana na Chadema katika kupinga vitendo hivyo kwani
kitendo hicho kinaumiza kila mtu.
Alisema iwapo Rais Magufuli
ataachiwa nafasi ya kukanyaga Katiba hakuna ambaye atapona au kuwa salama.
Mwenyekiti huyo alisema katika
kipindi kifupi cha Rais Magufuli kiburi na dharau imeonekana kutoka kwake na
watawala wengine badala ya kukaa na kuzungumza mema ya nchi hii ikiwemo amani.
Alisema viongozi hao wanahubiri
amani lakini matendo yao yanashiria uvunjifu wa amani na kinyume chake ni
kuandaa majeshi na kutesa viongozi, wanachana na watu wote ambao wapo kinyume
na mitizanmo yao.
Mbowe alisema uamuzi huo unaweza
kuwasikitisha wanachama wao lakini hakuna sababu ya kuingiza nchi katika
mgogoro ambao hauna sababu hivyo kuwataka wasubiri mazungumzo ya viongozi.
‘Hatuachi kuandamana kesho kwa
sababu ya Jeshi la Polisi au Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), ila
tumekubaliana kuheshimu viongozi wetu wa dini pamoja na ukweli kuwa rais
anawadharua, lakini ikifika Oktoba mosi tutaendeleza harakati zetu za kudai
haki,” alisema.
Kwa upande mwingine Mbowe alisema
katika kipindi cha mwezi mmoja wa maandalizi ya Ukuta viongozi na wanachama 230
wamekamatwa na kufunguliwa mashtaka maeneo mbalimbali nchini.
Halikadhalika alisema wabunge wa
Chadema, watarudi bungeni baada ya ombi la viongozi wa dini na kuwa wanatarajia
kukutana Dodoma kutafakari ushauri huo ili wawe na kauli moja ya kurejea.
0 comments:
Post a Comment