KIONGOZI
wa dini na viongozi wa makabila wamejitokeza kutaka suluhu katika mgogoro
unaoendelea baina ya Chadema kwa upande mmoja na Serikali na Polisi kwa upande mwingine.
Askofu wa
Jimbo Katoliki la Dodoma, Mhashamu Beatus Kinyaiya ametaka viongozi wa Chadema kutumia
uhuru walionao vizuri kukaa na Serikali meza moja kuelewana badala ya
kuhamasisha vijana washiriki maandamano ya Operesheni UKUTA yanayotarawa
kufanyika Septemba mosi.
Alisema
jana kwamba kama yatafanyika, upo uwezekano mkubwa maandamano hayo
yakasababisha madhara makubwa kwa jamii ya Watanzania. Askofu huyo alitoa kauli
hiyo alipozungumza na JAMBO LEO, baada ya kumaliza kutoa Sakramenti Takatifu ya
Kipaimara kwa watoto 111 wanafunzi wa shule ya Martin Luther mjini Dodoma.
“Kwa kuwa
washiriki wenyewe wa maandamano wengi ni vijana, kunaweza kutokea madhara mengi
yakifanyika. Tunajua kila Mtanzania ana uhuru wa kufanya kitu anachokifikiri kutokana
na uhuru uliopo nchini,” alisema na kuongeza:
“Lakini
naomba viongozi wa Ukawa kuutazama na kuutumia vizuri uhuru huo, hasa kukaa
meza moja na Serikali wakaondoa tofauti zilizopo.”
Alisema
moja ya madhara yanayoweza kujitokeza ni vijana wasio na nia nzuri kujiingiza
kwenye maandamano hayo, kisha kusababisha fujo, hali inayoweza kuathiri utendaji
kazi katika maeneo mengi na hasara kujitokeza kwa kuwa yanasemwa ni ya nchi
nzima.
“Kwanza
nasema kwa sababu ni Watanzania, kila mtu ana uhuru wa kufanya atakacho lakini
ni vema kama wangekutana na Serikali wakazungumza wakalimaliza mapema kuliko
kuacha mpaka wafike huko ambapo kunaweza kusababisha hasara kubwa,” alisema
Kinyaiya na kufafanua:
“Vijana ni
vijana, kwenye hayo maandamano yao wanaweza kuanza vizuri,†lakini vijana wenzao
walio na nia mbaya wanaweza kijichomeka na wakasababisha fujo.”
Kuhusu
hali ya kisiasa nchini, Askofu Kinyaiya alisema kutokuwa na mazungumzo ya
kutosha kati ya vyama vya siasa na Serikali kunasababisha vuguvugu la
kutazamana vibaya, hivyo ili kuondoa ukakasi huo kuwe na maelewano kati yao.
Shekhe
Alhad
Katika hatua
nyingine, Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum ametoa mwito
kwa viongozi wa kisiasa nchini, kuwa wavumilivu ili kulinda amani ya nchi.
Shekhe
Alhad alisema hayo jana ofisini kwake, Dar es Salaam akitaka viongozi hao kutii
Mamlaka iliyopo kwani imewekwa na Mungu na hivyo ni vema kutafuta njia nyingine
kumaliza matatizo yanapotokea.
“Ipo haja
ya kuvumiliana kwa ajili ya Taifa letu, kwani yanapotokea machafuko waathirika
wakubwa ni wanawake, watoto na vijana wetu ambao wanaweza kupata madhara
makubwa na hata kupoteza maisha,ÃÃalisema Alhad.
Akizungumzia
maandamano ya Ukuta yaliyopangwa kufanyika Septemba mosi, alisema kauli ya
kuzuia maandamano hayo ilitolewa na Rais wa Nchi na kuomba ipewe uzito wa
kipekee, kwani busara ni kusikiliza Mamlaka imesema nini na kutii kauli hiyo ya
Rais.
“Nawashauri
Watanzania wenzangu, viongozi wangu wa kisiasa jambo hilo si vyema tukashiriki
kwani kutotii Mamlaka ni dhambi ndivyo vitabu vya dini vinanavyosema,ÃÃ alifafanua
Shekhe Alhad.
Wazee Nao
wazee wa jamii ya kimasai wameiomba Serikali kukaa mezani na wanasiasa
wanaounda Operesheni Ukuta ili kumaliza hali inayojitokeza hivi sasa.
Akizungumza
kwa niaba ya jamii hiyo, Kiongozi Mkuu (Laibon), Masaine Kumunyu alisema hawako
tayari kushiriki jambo hilo kwani wanaitii Serikali. Alisema kwa muda mrefu
kumekuwa na malumbano kati ya viongozi wa kisiasa na Serikali ambapo walisema
kuna mambo wanaona hayafanyiki vema.
“Sisi
Wamasai hatuwezi kushiriki maandamano hayo, lakini pia tunaomba pande hizi kwa
maana ya Serikali na viongozi wa vyama vya kisiasa kukaa mezani ili kuzungumzia
mambo hayo na kuepusha madhara siku hiyo, Serikali inakataza, wanasiasa
wanasema azma iko palepale, kwa hali hiyo tunaziomba pande mbili hizi kukaa
mezani kuzungumza,” alisema Kumunyu.
0 comments:
Post a Comment