Na John Banda, Dodoma
WANAFUNZI wa Shule
ya Msingi ya Wasioona Buigiri Misheni iliyoko katika wilaya ya Chamwino mkoani
Dodoma, wamemwomba diwani wa kata hiyo Keneth Yindi greda la kusawazisha maeneo
ya shuleni hapo ambayo yamekuwa na mashimo na mifereji iliyokuwa ikipitisha maji
katika kipindi cha cha mvua.
Ombi hilo
limetolewa na wanafunzi hao walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari
waliotembelea shuleni hapo,baada ya kujionea jinsi wanafunzi wasioona
walivyokuwa wakitembea kwa tahadhari kubwa kutokana na hofu ya kutumbukia
kwenye mashimo na mifereji hiyo.
Mmoja wa wanafunzi
hao, Mariam John anayesoma darasa la sita mwenye uoni hafifu, alisema kuwa hivi
sasa wanafunzi wamekuwa wakianguka hovyo kwa kujikwaa na wengine kutumbukia
kwenye mifereji iliyokuwa ikipitisha maji.
Alisema kuwa
kutokana na hali hiyo wanamwomba diwani huyo greda kwa ajili ya kusawazisha
maeneo hayo ya shule ili wanafunzi waweze kutembea bila hofu ya kujikwaa na
hatimaye wengine kuanguka.
Alisema hivi sasa
kutokana na kuwepo kwa mashimo na mifereji hiyo, wanafunzi hao wamekuwa
wakitembea kwa tahadhari kwa kuhofu kuumia licha ya kupewa msaada na wezao
ambao wanaoona.
“Kwa kweli sisi wanafunzi tunamwomba diwani wetu atutupie jicho la
huruma ili turekebishiwe maeneo haya ya shule ambayo karibu sehemu nyingi kuna
mifereji na mashimo yanayotufanya tuwe tunajikwaa kwa s ababu ya kutoona kwetu,”
alisema..
Hata hivyo, wanafunzi hao walisema pamoja na changamoto hiyo,pia
wanakabiliana na uchakavu wa samani ya vifaa vya shule kama vile viti na meza,
huku kwa wale wanaotumia mashine ya nukta nundu wakichangia zaidi ya watatu hadi
wanne kwenye mashine moja.
Mwanafunzi Atanance Mathayo anayesoma darasa la tano alisema kuwa wanapeleka
maombi hayo kwa diwani huyo kutokana na umuhimu aliokuwanao wa kuchangia watu
wenye mahitaji mbalimbali. Alisema kuwa wao kuwa wanafunzi ni matumaini yao
diwani huyo anaweza kuwasaidia kama anavyoweza kutoa misaada mingine kwa watu
wengine.
0 comments:
Post a Comment