Mwandishi
Wetu
BARAZA
Kuu la Chama cha Wananchi (CUF), linatarajia kukutana siku chache zijazo
kujadili pamoja na mambo mengine, hatima ya uanachama wa aliyekuwa Mwenyekiti
wake, Profesa Ibrahim Lipumba na wafuasi wake.
Wengine
ambao wanatarajiwa kujadiliwa uanachama wao ni Naibu Katibu Mkuu Bara, Mbunge
wa Kaliua, Magdalena Sakaya, Mbunge wa Mtwara Mjini Maftah Machuma, Thomas Malima,
Ashura Mustapha na Naibu Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano, Abdul Kambaya na
wengine wengi.
Taarifa
ambazo JAMBO LEO ilizipata kutoka chanzo cha uhakika ndani ya CUF, zilisema
maandalizi ya vikao vya wazee ambao watajadili sakata hilo ambalo linaweza
kusababishamigogoro ndani ya chama yanaendelea.
Mtoa
habari huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe,
alisema wamekusanya ushahidi wa kutosha kuhusika kwa watu wa CCM,
hivyo wanatarajia kufanya uamuzi mgumu
ambao utakiacha chama kikiwa salama.
“Sisi
tumepata ushahidi wote kuiwa watu wa CCM wanatuma fedha kwa mitandao ya simu
kwa watu wetu, hivyo tumeamua kuwapa nafasi wazee ili wapitie hatua kwa hatua
na tutaitisha Baraza Kuu Maalumu, ili kufanya uamuzi,” alisema.
Mtoa
habari huyo alisema utaratibu anaoutumia Profesa Lipumba haukubaliki kwani
lengo lake ni kuvuruga chama huku akisisitiza kuwa CUF inaweza kuendelea kuwa
imara bila yeye.
Alisema
Profesa Lipumba amediriki kumwambia Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad kuwa atahakikisha
anarejea CUF kwa njia yoyote la sivyo chama kife.
“Hakuna
sababu ya kubaki na mnafiki anajaribu kutupotezea muda, aliondoka katika
kipindi kigumu na akasema anakwenda kufanya uchambuzi wa uchumi, sasa anataka
kurudi kwa fujo haikubaliki,” alisisitiza.
Alisema
ushahidi wa CUF kupata mafanikio upo kwani aliondoka wakiwa na wabunge wawili
wa kuchaguliwa na sasa ni 10 na inaongoza baadhi ya majiji na halimashauri. Profesa
Lipumba alijiondoa kwenye wadhifa wa uenyekiti wa chama hicho mwaka jana
akipinga kupokewa kundini (UKAWA) kwa Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa na
kusimamishwa kugombea urais kwa tiketi ya Chadema kuungwa mkono pia na Ukawa.
Hata
hivyo, alibwagwa na mgombea wa CCM, Dk John Magufuli ambaye hivi sasa ni Rais wa
Awamu ya Tano.
Baada ya
kushindwa, hivi sasa Lowassa ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema na anaongoza Operesheni
Ukuta kanda ya Nyanda za Juu Kusini.
Hivi
karibuni, Profesa Lipumba alibadili mawazo na kuomba kurejea ulingoni akitaka
kugombea uenyekiti wa chama hicho, hatua ambayo imesababisha mgawanyiko ndani
ya chama hicho, hata kuvuruga Mkutano Mkuu maalumu uliofanyika juzi Dar es Salaam.
Maalim
lawamani
Naye
Emeresiana Athanas anaripoti kwamba, siku moja baada ya Mkutano Mkuu wa CUF, kuvunjika
kutokana na mvurugano uliotokea baadhi ya wanachama wamedai kilichotokea ni
mipango ya Katibu Mkuu wa Chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad kukivuruga.
Taarifa za
ndani ya chama hicho zilieleza kuwa hadi sasa wanachama zaidi ya 300 wakiwamo wajumbe
wa Kamati Kuu wamejitokeza kupinga matokeo ya upigaji kura wa kukubali au
kukataa kujiuzulu kwa Profesa Lipumba ndani ya CUF.
Mvurugano
huo ulitokea juzi katika ukumbi wa Blue Pearl Ubungo kwenye mkutano huo wa
dharura kwa ajili ya kupokea taarifa na kufanya uchaguzi wa kuziba nafasi za
Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho zilizoachwa wazi.
Walitoa
madai hayo Dar es Salaam jana, wakati wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti
wakidai mkutano huo haukufanyika kihalali kutokana na sehemu ya wanachama zaidi
ya 100 kuingia kinyume na utaratibu.
Hata
hivyo, taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na chama hicho kupitia
Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma, Salim Bimani ilisema pamoja na
kuahirishwa kwa mkutano huo kutokana na vurugu kitatoa taarifa ya marudio ya
mkutano kwa ajili ya kuziba nafasi zilizo wazi.
0 comments:
Post a Comment