MWENYEKITI wa Chama Cha
NCCR-Mageuzi, James Mbatia amesema mazungumzo ya mpango wa kuunda chama kimoja
cha siasa cha upnzani nchini yanaendelea na kwamba mkakati huo unafanyika kwa
vitendo bila maneno.
Hata hivyo, Mbatia mabaye
pia ni mwenyekiti mwenza wa Umoja wa Vyama Vinavyounda Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa), amekiri kuwa changamoto iliyopo katika kuunda chama hicho ni
suala la uaminifu aliosema inabidi uwepo baina yao kabla ya mchakato huo
kufanyika.
Mbatia alitoa kauli hiyo
jana wakati akihojiwa kwenye kipindi cha Funguka kupitia Kituo cha Televisheni
cha Azam Two kinachoendeshwa na mtangazaji mahiri Tido Mhando.
"Mazungumzo ya kuwa
na chama kimoja yanaendelea kwa vitendo bila maneno maana mtihani wa kwanza ni
bungeni kuwa kitu kimoja, lazima tuwe kitu kimoja, "alisema.
Alisema kila chama cha
siasa kimesajiliwa na ndio maana kinaendesha majukumu yake kama kawaida na
yakiwepo mambo ya pamoja lakini hukutana kujadilikwa pamoja ili kupata mwafaka
ya yanayowahusu na kuwaunganisha.
Mbatia alisema
wanaovihukumu vyama vya upinzani kwa kutokuwa na umoja kwa sasa hawawatendei
haki akisema ni mapema na kusisitiza kwamba mchakato huo wa kuunda chama hicho
unaendelea.
"Kutuhukumu ndani ya
miezi minane tuu baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu, kutuhukumu namna hii
mnakuwa hamtutendei haki hata kidogo,"alisema.
Alisema zipo kanuni
bungeni na maandishi mbalimbali ndani ya ukawa kupitia kamati kuu ya Ukawa ,
kamati ya makatibu wakuu , na kamati ya ukawa ambayo huwa wanakaa pamoja
kuzungumza mambo yanayohusu umoja huo kwa utaratibu.
Alisema suala la
kuaminiana ni jambo la msingi ndani ya umoja huo kwani kuujenga kunahitaji
utashi zaidi wakizingatia umuhimu wake na tija kwa Taifa.
"Mimi kukuamini wewe
na wewe kuniamini mimi kwa mfano Mwalimu Julias Nyerere mwaka 1962 alikaa na
Karume alikuwa na utashi wa kukaa pamoja ii kujadili namna ya kuunganisha
Zanzibar wawe kitu kimoja," alisema.
Alisema suala hilo
lilikuwa tendo la maridhiano kati ya pande mbili na kwamba ndio sababu
lilifanikiwa kutokana na kuwepo kwa kuaminiana na baada ya siku mbili suala
hilo lilifanyika na nchi ikapata Muungano.
Aliongeza kwa hata muafaka
wa Zanzibar ulianza kati ya Mzee Amani Karume na aliyekuwa Rais kipindi hicho
na Maalim Seif Sharrif Hamad, hivyo umainifu wa viongozi hao n kuaminiana kwao
inaleta viongozi.
Mbatia alisema wakati
wanaanzisha ukawa lengo lao lilikuwa ni kuwa na umainifu na kwamba mazungumzo
yalikuwepo ambapo walifanya mtihani huo mwaka jana na kufanikiwa kumteua
mgombea mmoja kupitia umoja huo
Alisema japo kuna sehemu
nyingine kwenye majimbo waliyogawana kuliibua fikra na mijadala tofauti.
Mbatia alisema uwezo wa
kuunda chama kimoja upo pale pale na waanamini kuwa watashinda.
Ukawa kunufaisha Chadema
Mbatia alionekana kukwepa
swali kuhusu Ukawa kufaidisha Chadema, badala yake alisema kuwa NCCR 'unaweza
kuwa na fikra hizo lakini nilisema mwanzoni kuwa hekima ni ule uwezo anaopewa
mwanadamu wa kufanya maamuzi yenye busara kwa kutumia uzoefu pamoja na taarifa
sahihi'.
Alisema si kwamba chama
kinachotoa mgombea urais ndiyo kinapata maslahi zaidi kuliko kingine, bali
kinachoangaliwa ni maslahi na kukuza utu wa Watanzania.
Alisema shabaha yao kubwa
si kupambana na CCM pekee bali kuona ustawi wa Tanzania, watu wake wakiwa na
elimu shirikishi, bora na kwa wote.
Alipoulizwa kama hana
wasiwasi kwamba chama chake kitadhoofika
katika Ukawa Mbatia alisema: “Ninaamini changamoto tulizonazo ndani ya
chama changu na migogoro ya kifikra inatuimrisha tuzidi kuipotezea.”
Alisema ingawa watu
wanaweza kuona kama NCCR imedhohofika lakini ni msaada kwa Ukawa ili
kuwaunganisha wapinzani pamoja.
Akwepa kuzungumzia Ukuta
Kiongozi huyo pia
alipotakiwa kueleza kama anaunga mkono
Operesheni ya Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (Ukuta), alisema yeye si
msemaji mkuu wa Chadema .
Alisema kwakuwa Chadema ni
washirika ndani ya Ukawa na wanachozungumzia ndani ya Ukuta ni kupinga uonevu
ni kutaka taratibu zifuatwe hususani katiba inayopingwa kwa sasa iweze
kutekelzwa ibara ya 20.
Alifafanua kuwa Ibara hiyo
inazungumzia haki ya watu kujumuika, kuzungumza kuweza kushiriki katika uhuru
wa kauli.
Mbatia alisema kuwa
inahitajika meza ya maridhiano ili changamoto zilizopo nchini zimalizike.
0 comments:
Post a Comment