*Bodi ya wadhamini yatambuliwa rasmi na Rita
*Ni
iliyo upande wa Mwenyekiti Prof. Lipumba
Celina Mathew
Lipumba na Maalim Seif |
WAKALA wa Ufilisi na Udhamini (Rita), umeidhinisha
Bodi Mpya ya Wadhamini ya CUF, huku chama hicho kikitarajia kufuta kesi zilizo mahakamani
zilizofunguliwa na Bodi iliyopita ikiwamo ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis
Mutungi na viongozi wake wengine ikieleza kuwa mgogoro uliokuwapo umemalizika.
Aidha, CUF chini ya uenyekiti wa Profesa
Ibrahim Lipumba, imemtaka Katibu Mkuu wake, Maalim Seif Sharrif Hamad kusamehe
yaliyopita na badala yake aende ofisi ya makao makuu Buguruni kuendelea na kazi
za kukijenga upya chama.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu
wa Bodi hiyo, Thomas Malima alisema usajili wa Bodi hiyo ni kwa mujibu wa
sheria ya udhamini na ya muunganisho wa wadhamini sura ya 318 toleo la 2002.
Alisema kwa mujibu wa sheria namba tano
ya mwaka 1992 ya usajili wa vyama vya siasa, inataka kila chama kilichosajiliwa
kuwa na Bodi ya Wadhamini iliyosajiliwa na Rita na inaishi kwa mujibu wa Katiba
na sheria za nchi.
Kwa mujibu wa Katiba ya CUF ya mwaka 1992
toleo la 2014 ibara ya 98(1) Bodi ya Wadhamini ya CUF itadumu kwa miaka mitano
kisha itateuliwa nyingine kwa kutumia sheria ya muunganisho wa wadhamini sura
ya 318, toleo la 2002
Aliongeza kuwa mjumbe wa Bodi hiyo
anaweza kuteuliwa tena na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa baada ya muda wake
kumalizika.
Alisema Bodi hiyo kwa kawaida huundwa na
wajumbe tisa ambapo watano kati yao lazima watoke Tanzania Bara na wajumbe wanne
Zanzibar ambapo mmoja anapaswa kuwa mwanamke na hiyo ni kwa mujibu wa Katiba ya
Chama hicho ibara ya 98 (2).
Alisema majukumu ya kikatiba ya Bodi
hiyo ni kudhamini fedha na mali za chama na madeni, pia ndiyo yenye mamlaka ya
kushitaki au kushitakiwa kwa niaba ya chama.
Malima alifafanua, kuwa upembuzi
yakinifu uliofanywa na Rita, ulibaini uhalali wa mabadiliko ya Bodi hiyo kuwa
yamekidhi matakwa ya Katiba ya CUF ambapo Juni 12 walikiandikia chama barua.
“Tuliandikiwa barua rasmi ya
kutufahamisha kuwa wamejiridhisha kwamba wadhamini walioteuliwa walikidhi
vigezo vya udhamini na hivyo kuwasajili rasmi,” alisema.
Alisema baada ya kupokea barua hiyo ya
Rita, wao Bodi ya Wadhamini walikaa na kuazimia kuwa yeye aandike barua kwa
benki zote zenye akaunti za CUF nchini, kuzitaka ziruhusu miamala ya kuweka na kutoa
fedha za chama kwa kuwa ndiyo halali inayotambuliwa na Rita.
Aliongeza kuwa Bodi hiyo imeteua watia
saini wapya wa akaunti zote za CUF ngazi ya Taifa na imethibitisha akaunti ya
CUF ya benki ya NMB tawi la Temeke kuwa akaunti ya wadhamini ngazi ya Taifa.
Alitoa hadhari kwa wanachama wanaojiita
Kamati ya Uongozi ya Taifa kuacha mara moja na wakisikika wanajivika nyadhifa
hizo watachukuliwa hatua na Bodi ya Wadhamini.
Kesi
Katika hatua nyingine, chama hicho
kinatarajia kufuta kesi zilizofunguliwa kwenye mahakama mbalimbali nchini na
iliyokuwa Bodi ya Wadhamini ya CUF dhidi ya Msajili wa Vyama vya Siasa,
Mwenyekiti wa Chama, Kaimu Katibu Mkuu na viongozi wengine.
“Ijumaa (kesho) tutaanza kufuta kesi
mbili zilizofunguliwa na Bodi iliyopita pia tumeondoa mawakili wote wa mwanzo
kwenye mahakama zote, tumeweka wapya na sasa wanaendelea na kazi wakifuatilia
masuala mbalimbali yakiwamo ya kesi za wizi wa ruzuku za chama na inayomhusu
Msajili,” alisema.
Mkurugenzi wa Habari wa CUF, Abdul
Kambaya alisema chama hicho kimeteseka sana na mgogoro uliokuwepo, lakini kwa
kuwa sasa Bodi mpya imepatikana changamoto hiyo itakwisha.
“Tumeteseka sana, wanachama wameumia
kujenga chama, lakini wenzetu wenye uchu wa madaraka wakakitupa na kuunga mkono
mafisadi, kwa sasa CUF tuko tayari kuanza upya kuliko kuendelea kubomolewa,” alisema.
0 comments:
Post a Comment