Celina Mathew
David Kafulila |
ALIYEKUWA Mbunge wa Kigoma Kusini, David
Kafulila amelaani hatua ya Mkuu wa Wilaya ya Hai, Gelasius Byakanwa kutumia
mamlaka yake kuvamia na kuharibu shamba la Mwenyekiti wa Chadema, Freeman
Mbowe.
Juzi, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya
hiyo ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya walivamia shamba la Mbowe nyumbani kwake
Machame na kuharibu miundombinu, mali, mboga na mimea kadhaa.
Akizungumza Dar es Salaam juzi, Kafulila
alisema amesoma na kusikia kuwa Mkuu huyo alitumia mamlaka yake kufanya kitendo
hicho, jambo ambalo aliliita ni laana ya hali ya juu.
“Nimesoma na kusikia kuwa Mkuu wa Wilaya
ametumia mamlaka yake kuvamia na kuharibu shamba la Mwenyekiti wa Chadema
ambalo ni uwekezaji wa kilimo cha mboga kwa soko la ndani na nje ya nchi,” alisema.
Alisema kitendo hicho ni cha kushangaza,
kwa kuwa shamba hilo lina thamani ya mamilioni ya fedha, lakini mtu anatokea na
kuharibu miundombinu kwa kuwa ni kiongozi tena bila sababu za msingi jambo
ambalo halileti picha nzuri kwa jamii.
“Huu ni uamuzi unaoweza kufanywa na
Serikali za kishenzi kama Somalia au Sudani na Burundi. Nasita kuamini kama
huko ndiko Rais John Magufuli anataka kutupeleka,” alisema na kuongeza:
“Naamini atachukua hatua kali dhidi ya
DC huyu, kwani ni doa lenye viashiria vya chuki za kisiasa kwa kiwango cha
unyama, chuki ambayo hakika sidhani kama inaweza kuwa maelekezo ya kiongozi anayemtaja
Mungu na kuomba maombi siku zote.”
0 comments:
Post a Comment