Dalila Sharif
Wilaya ya Temeke |
WAKAZI
wa wilaya za Temeke na Kigamboni wameiomba Wakala wa Huduma za Misitu (TSF)
kuwashirikisha kwa kuwapa elimu ya utunzaji mazingira ili kunufaika nayo katika kulinda mazao
yake, kuzuia uchomaji mkaa na ukataji miti ovyo.
Wakizungumza
Dar es Salaam jana kwa nyakati tofauti, wananchi hao walieleza wanavyotambua
wajibu wao katika utunzaji mazingira.
Mmoja wa
wakazi hao kutoka Temeke, Mariam Swedi alisema ni wajibu wa kila mwananchi
kushirikishwa katika utunzaji mazingira ya misitu kama mazao, uoto wa asili, nyuki,
bustani na aina zingine.
“Hali
hii imejitokeza kwa baadhi ya wakazi wa Dar es Salaam kukosa mwamko wa
kushirikishwa katika utunzaji na ulinzi wa misitu yetu hivyo kusababisha
wachache kunufaika nayo kwa uvunaji holela wa mazao ya misitu,” alisema Mariam.
Mkazi wa
Kigamboni, Burhani Kambi alisema zipo baadhi ya sehemu wananchi hunufaika na mazao
ya misitu hivyo hushirikisha wananchi ni jambo la msingi ili kuilinda na
kuitunza, wavunaji haramu wasivamie na kuiba mazao na kukata kuni au kuchoma
mkaa.
“Kwa nini
wananchi tunaoishi mijini hatushirikishwi kulinda na kuitunza hata kunufaika nayo
hali ambayo inabaki kusimamiwa na mawakala wa misitu pekee; watushirikishe nasi
tunaweza kuiendeleza kama vijijini ambako wananchi wanajumuika kuitunza na
kuwaingizia mapato,” alisema Kambi.
Pamela
Oscar wa Kigamboni alisema ingawa wilaya hiyo imejaaliwa neema ya misitu kama
wa Mwandege, wananchi wanastahili elimu ya juu ya umuhimu wa misitu na kuacha uharibifu
wa ukataji miti ovyo pembezoni mwa wilaya hizo.
0 comments:
Post a Comment