Mary mtuka
Hamis Kigwangalla |
NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Hamisi Kigwangalla amekabidhi jumla ya vifaa 831
vyenye thamani ya jumla ya Sh. milioni 400, kwa kituo cha Afya Mkoani Kibaha
Mjini, vifaa vilivyotolewa na Mbunge wa jimbo hilo, Silvestry Koka.
Kabla ya kukabidhi vifaa hivyo, Dk.
Kigwangalla alikagua maeneo ya majengo ya kituo hicho na kubaini mambo
mbalimbali aliyoagiza yafanyiwe kazi ili kituo hicho kiweze kuwa Hospitali ya
Wilaya.
Dk. Kigwangalla alipongeza juhudi za mbunge
huyo kujali wananchi wake kwani hadi kuweza kupata vifaa hivyo aliweza kutumia
maarifa na ukaribu wake na wananchi wake hivyo kufika kwa vifaa hivyo vitakuwa
faraja kubwa kwa Wanakibaha na wananchi wote wa maeneo jirani.
“Nampongeza Mbunge Koka kwa kuwaletea
vifaa hivi ni vizuri na vitakuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa Kibaha na maeneo
yake ya jirani. Nakupongeza sana,” alieleza Dk. Kigwangalla.
Kwa upande wake, Mbunge huyo amemshukuru
Naibu Waziri Dk. Kigwangalla kwa kuweza kufika na kujionea kituo hicho sambamba
na kukabidhi vifaa huku akimuomba kuendelea kufika mara kwa mara kujionea
mipango ya afya jimboni humo.
“Leo hii najisikia faraja baada ya vifaa
hivi kufika hapa jimboni kwangu kutoka
nchini Marekani. Nawaomba vitumike kwa uangalifu mkubwa sana na viweze kuwa
msaada kwetu,” alisema.
Alisema Halmashauri ya Kibaha imechangia
Sh. milioni 32 ambazo zimesaidia
usafirishaji wa vifaa hivyo kutoka nchini Marekani, huku Mbunge akitumia Sh.
milioni 12 kwa ajili ya kuwaleta wataalamu kwa ajili ya ukaguzi na kuvifunga
vifaa hivyo.
Mbunge huyo alisema vifaa hivyo
vitagawia katika zahanati na vituo vyote vilivyopo mjini Kibaha na maeneo
mengine yenye uhitaji.
0 comments:
Post a Comment