*Ni kwa juhudi zake za kupigania rasilimali za nchi
*Amwombea ushirikiano ili Watanzania wale siagi kama Wazungu
Seif Mangwangi, Arusha
Rais John Magufuli akiwa bandarini |
ASKOFU
Mkuu wa Kanisa la International Evangelism Church (IEC), Sakila la Arumeru
jijini hapa, Dk Eliud Issangya amemwelezea Rais John Magufuli, kuwa ‘mwanamume
shujaa na mzalendo’ kutokana na hatua anazochukua za kupigania rasilimali za
Tanzania.
Akizungumza
jana jijini hapa, Askofu Issangya alisema Kanisa lake linampongeza Rais
Magufuli kwa kuzuia usafirishaji mchanga wa dhahabu na kumtaka kuhamishia
mapambano hayo kwa wabadhirifu wa rasilimali za nchi katika sekta za
wanyamapori, mafuta na gesi.
Alisema
sekta za wanyamapori, mafuta na gesi hazina tofauti na sekta ya madini, hivyo
Rais hana budi kufuatilia nyendo katika sekta hizo na kuzuia wizi unaoendelea
kufanywa kwa miaka mingi sasa.
“Ni
miaka miwili sasa, tangu Rais Magufuli achaguliwe, lakini ameonesha yeye ni
mzalendo namba moja na shujaa wa kupigania rasilimali za Tanzania.
“Kaonesha
ulimwengu kuwa rasilimali hizo ni za Watanzania na si za Wazungu, sisi
tunakupongeza Rais, wewe ni mwanamume, hakika umethubutu,” alisema Askofu
Issangya.
Alisema
Dk Magufuli ni kiongozi anayestahili kuigwa na kutoa mwito kwa Watanzania
kuungana kumwombea afya njema, ili afanikishe malengo aaliyojiwekea ikiwamo
kuzuia wizi wa rasilimali za nchi.
Askofu
Issangya alisema uzalendo anaoonesha Dk Magufuli hivi sasa, kwa miaka ijayo
Tanzania itakuwa miongoni mwa nchi tajiri duniani na bei ya vitu muhimu
kama vyakula na mafuta itashuka.
“Rais
akiendelea na kasi hii hii, kama Kanisa tunaamini umasikini utakwisha kabisa na
kwanza umeshaanza kwisha, kila Mtanzania atakula siagi kama Wazungu wanavyokula
na hii ni kwa sababu Rais ameamua kusema basi imetosha,” alisema.
Aliwataka
wapinzani kuungana na Rais na kuacha kupinga juhudi alizoanzisha, kwa kuwa
kufanya hivyo ni kumkatisha tamaa na matokeo yake ni kurudisha nyuma jitihada
anazofanya na kulifanya Taifa kuendelea kuwa masikini licha ya utajiri uliopo.
Katika
hatua nyingine, Askofu Issangya alimwomba Rais kuwapa wachimbaji wadogo maeneo,
ili kupunguza migogoro ambayo imekuwa ikishuhudiwa kutokea mara kwa mara
wakigombana na wachimbaji wakubwa.
Askofu
Issangya katika kikao hicho alifuatana na msaidizi wake, Mchungaji Gabriel
Maasa, Askofu Gerald Mollel wa IEC Kilimanjaro Magharibi na Askofu Michael
Laizer wa Arusha Mashariki. Pia aliwapongeza wasaidizi wa Rais; Makamu wa Rais,
Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
0 comments:
Post a Comment