Celina Mathew
David Kafulila |
MBUNGE wa zamani wa Kigoma Kusini, David
Kafulila, ametaja vikwazo viwili vinavyosababisha nchi kukosa mikopo wa wahisani
ya kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo iliyopangwa tangu mwaka jana hadi
sasa.
Vikwazo hivyo ni mgogoro wa Zanzibar, ukandamizaji
wa demokrasia na vikwazo kwa wafanyabaishara huku akiishauri Serikali
kuhakikisha inamaliza changamoto hizo na kupata mikopo ya bei nafuu.
Akizungumza jana baada ya taarifa ya
Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) kuhusu mwenendo wa Uchumi na Bajeti
Tanzania iliyotolewa hivi karibuni Kafulila alisema Bajeti ya Mwaka 2017/18
haitatekelezeka kama nchi itaendelea kukosa mikopo ya nje.
Alisema Serikali inapaswa kushughulikia
mgogoro wa Zanzibar na kusitisha ukandamizaji wa demokrasia ili iendelee kupata
mikopo nafuu kwani ni moja ya vigezo vya kupata mikopo hiyo.
Alisema Tanzania inaweza kupata mikopo
nafuu ya hadi dola bilioni 2.5 sawa Sh trilioni 6 kwa mwaka, ambapo ni kiasi
cha kutosha kwa Serikali kumudu miradi ya kimkakati kama ujenzi wa reli, umeme
na bandari.
Pia, lazima Serikali ikae na
wafanyabiashara na kuwahakikishia kwamba Tanzania ni sehemu salama kuwekeza na
hivyo waweze kuingiza mtaji zaidi, kwani uchumi wa viwanda hauwezi kujengwa
kama haipatikani mitaji kutoka kwenye Uwekezaji wa Moja kwa Moja wa Nje (FDI ).
Kafulila alisema kwa muda sasa kwa nchi
imekuwa vigumu kupata mikopo nafuu kutokana na masharti yake ya demokrasia na
utawala bora.
Alisema mikopo ya kibiashara kutoka nje imeendelea
kuwa migumu kutokana na taasisi za kimataifa kuanza kuisoma Serikali kuwa si
rafiki wa mazingira ya biashara.
Aliongeza kuwa mbaya zaidi hatujafanya riba
za mikopo ili kuhakikishia wawekezaji na benki kwa maana ya kupata mikopo kama
ilivyokwishafanyika Kenya na Rwanda kwa upande wa Afrika Mashariki.
“Mazingira yalivyo ni vigumu kupata
mkopo kuendesha bajeti na ndiyo maana Serikali imezidi kukopa ndani na kufanya
deni la ndani kwenda juu na kuvunja rekodi tangu awamu ya tatu,” alisema.
Alisema awamu ya tatu iliacha deni la
ndani la Sh trilioni 1.7, miaka 10 ya awamu ya nne deni la ndani lilifikia Sh
trilioni 7.5 mwaka juzi, sasa miaka miwili tu, deni limefika zaidi ya Sh trilioni
sawa na nyongeza ya Sh trilioni 3.5 kwa miaka miwili.
“Hii ni hatari sana kwenye nchi ambayo
mzunguko wa fedha ndani uko chini mno. Hali ikibaki ilivyo, nchi itazidi kuzama
kiuchumi kwa kushindwa kugharimia mahitaji ya afya, maji na elimu kwa sababu
ukiangalia deni lililoiva mwaka jana ilikuwa Sh trilioni 8 wakati mwaka huu ni
Sh trilioni 9.
Alisema wakati deni hilo likiongezeka
hadi Sh trilioni 9 bado mshahara ni Sh trilioni 7.6 na kwamba hiyo inamaanisha
kuwa jumla inakuwa ni Sh trilioni 16.6.
Alisema katika mazingira ya sasa ambayo
kodi inayokusanywa kwa mwezi na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ni wastani wa Sh
trilioni 1.1 hadi Sh trilioni 1.2, si zaidi ya Sh trilioni 14 kwa mwaka.
Alisema hiyo inamaanisha kwamba
makusanyo ya kodi hayatoshi kumudu deni la mshahara kwakuwa tunakopa kwa ajili
ya kulipa mishahara wakati gharama za kuendesha serikali na miradi ya maendeleo
haijazungumziwa.
Alitolea mfano China ambayo ni Taifa la
pili kwa ukubwa wa uchumi duniani baada ya Marekani ambazo pamoja na msimamo
wake wa Ujamaa, imefikia ilipo kwa kuwa nchi ya pili baada ya kuwekeza zaidi
kwenye elimu, ufundi na teknolojia.
Alisema mtaji mkubwa uliojenga uchumi wa
China ulitoka nje hususan Marekani na kwamba lazima ujengwe uchumi wa kisasa
kwa kuangalia maendeleo ya dunia na kurekebisha mazingira ya kibiashara.
Alisema mazingira hayo yakirekebishwa na
kujengwa imani kwa wawekezaji, mitaji na mikopo itapatikana zaidi ili kuelekea ndoto
ya Dira ya Taifa ya Mwaka 2025.
Aliongeza kuwa kwa mujibu wa taarifa ya
Poverty and Human Development ya mwaka 2014 ili tufikie dira hiyo, lazima
pamoja na mambo mengine tuajiri walimu 900,000 sawa na wastani wa walimu 90,000
kila mwaka.
“Leo ajira za walimu tumeajiri sana
mwaka juzi hawakuzidi 30,000, kilimo kinachoajiri asilimia 70 sasa kinakua kwa
asilimia 1.7, kiasi ambacho nchini kupata kutokea tangu Uhuru,” alisema.
0 comments:
Post a Comment