Mary Mtuka
Teknolojia |
VIJANA wametakiwa kutumia teknolojia ya
mawasiliano katika kupata fursa mbalimbali, ikiwemo sera zinazoendesha nchi na
hatimaye kujikwamua kimaisha.
Mwito huo umetolewa na Mgunduzi wa Mtandao
wa Platform for Policy Engagement (PUPE), Farhan Yusuf katika semina ya
kuwajengea uwezo vijana na kusikiliza matatizo yao mwisho mwa wiki Dar es Salam.
Alisema mitandao hiyo ikitumika ipasavyo
kwa vijana ni wazi kuwa watakuwa na uwelewa mzuri na hatimae kujikwamua
kiuchumi.
Yusuf alisema kutokana na changamoto
kubwa ya uwelewa mdogo wa matumizi ya mitandao ameamua kuazisha PUPE ili
kusainia vijana.
"Lengo langu kubwa la kuazisha
mtandao huo ni kuwasaidia vijana kupata fursa ya kujifunza sera na Sheria na
mambo mbalimbali yatakayo tumika katika kuiendesha nchi," alisema.
Aliongeza kuwa asilimia kubwa ya vijana
wanaokaa vijiweni wamekuwa wakilalamika huku wakiwa hawajui sera wala miongozo ambayo
inahusu mitandao.
Mkurugenzi Mwenza wa
Taasisi ya Sahara Sparks,
inayojihusisha na kuwajengea uwezo
vijana katika miradi mbalimbali ya kiteknolojia, Muda Kamata alisema wamejipanga kuwawezesha vijana
hao kuazisha mitandao mingi zaidi.
Alisema pamoja na changamoto zinazowakabili
vijana wemeona upo umuhimu wa kutumia njia ya mitandao ili kuweza kujua
michanganuo mbalimbali ya kijamii kutokana na kuendelea kukuza kwa teknolojia.
Kwa upande wake Msimamizi wa Mawasiliano
kutoka Kampuni ya Teknolojia ya CIPESA,
ya nchini Uganda Bassil Malaki alitumia fursa hiyo kuwa sisitiza viongozi
kutumia mitandao, kwani itasaidia kutatua kero za wananchi kwa wakati.
0 comments:
Post a Comment