Mwandishi Wetu
Waziri Mpango |
MBUNGE wa Tunduma, Frank Mwakajoka
(Chadema), amewataka wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuacha usanii katika
masuala ya Kitaifa akisema wanachofanya wanaumiza wananachi hasa wa vijijini.
Mwakajoka amesema iwapo Taifa lingekuwa linaendeshwa
kwa misingi ya uadilifu na uwajibikaji Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip
Mpango angeapaswa kujiuzulu.
Alisema pamoja na Serikali kushindwa
kutekeleza Bajeti zilizotengwa katika maendeleo takribani miaka, yote bado
wabunge wa CCM wamekuwa wakiunga mkono na kupongeza.
Alisema katika Bajeti ya 2016/17 zaidi
ya Sh. trilioni 11 fedha zilizoenda katika miradi ni Sh. trilioni 4 sawa na
asilimia 38 jambo ambalo linaashiria kuwa utekelezaji ni tatizo.
“Hapa bungeni tulitenga Bajeti ya
maendeleo katika kilimo sh. bilioni 101 fedha zilizoenda ni Sh. bilioni 3,
umwagiliaji ilitengwa Sh. bilioni 35 ila imeenda Sh. bilioni 1 jambo ambalo
liaashiria kuwa hakuna nia ya kutatua changamoto za nchi,” alisema.
Alisema mwaka 2015/16 wakati wa Serikali
Rais mstaafu Jakaya Kikwete alitenga zaidi ya Sh. bilioni 88 kwa ajili ya
pembejeo za kilimo ila leo wametenga Sh. bilioni 10 halafu wanapongeza
Serikali.
Alisema ni jambo la kusikitisha kuona
serikali inakimbilia kutoa mabilioni ya fedha kununua ndege wakati hali ya afya
ni mbaya nchini.
Mwakajoka alisema Watanzania hawajawahi
kusema wanahitaji ndege na reli hivyo Serikali ingepaswa kujikita katika sekta
ambazo zinasaidia jamii kubwa kama kilimo.
Alisema uwekezaji ukielekezwa katika
kilimo, mifugo na uvuvi ni kundi kubwa ambalo litafaidika kwa haraka hivyo
dhana ya uchumi wa viwanda itaanza kutimia kwa haraka.
“Napenda kusema katika kipindi hiki
tunapaswa kuwekeza kwa wafugaji, wavuvi na wakulima kwani takwimu zinaonesha
kuwa kundi hilo ni asilimia 75 ya Watanzania,” alisema.
Alisema ufinyu wa Bajeti katika sekta ya
viwanda itakwamisha mpango wa kuleta viwanda hivyo kuwataka wabunge waachane na
utamaduni wa kusema ndio kwa kila jambo.
Akizungumzia hoja ya kumtaka Waziri
Mpango kuwajibika kwa kile alichodai kuwa ameshindwa kusimamia wizara alisema
wakati wananchi wakitambua kuwa wana mchumi ameanza kuingiza wamachinga kulipa
kodi.
Alisema waziri angepaswa kuja na hoja
yenye tija kwa nchi na wananchi na kuwa kuwahusisha wamachinga katika kodi ni
kupoteza mwelekeo.
“Katika dunia hii ulishaona wapi
wamachinga wakilipa kodi mabya zaidi hamjaweka mazingira rafiki ya watu hao
kufanya biashara wakiwa huru,” alisema.
Aidha, Mbunge huyo ametoa angalizo kwa
Serikali kutaka kumchunguza na kuwashtaki waliokuwa wanasheria wakuu katika
suala la mchanga wa madini (makinikia), kwa kile alichodai kuwa hakuna ambaye
atabakia salama.
0 comments:
Post a Comment